Skip to main content

ZIJUE TOFAUTI KATI YA VIVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI(FIBROIDS) NA VIVIMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI(OVARIAN CYSTS).

Vivimbe vyote katika ya fibroid na ovarian cysts huwa ni kawaida kwa wanawake, hasa kabla ya kukoma hedhi.  
 




Vivimbe kwenye mfuko wa uzazi huwa ni aina uvimbe mgumu ambao hujengeka kwenye msuli wa ukuta wa tumbo la uzazi(uterus). Kinyume chake, vivimbe maji kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) huwa ni vifuko vyenye majimaji ambavyo huendelea kukua ndani au juu ya vifuko vya mayai.

NUKUU: Na licha ya kutokea sehemu mbalimbali, dalili pekee zinaweza kukuacha ukashangaa kitu gani kibaya.  
 
Hebu tuangalie mifano yake na tofauti kati ya vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts). Tutaelezea pia kwanini ni muhimu sana kufanya vipimo.



JE, DALILI ZA UVIMBE WA FIBROID NA VIUMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI ZINAKUWA JE? 
 
Vivimbe vya fibroid na ovaria cysts mara nyingi huwa havisababishi dalili. Unaweza usitambue kama una vivimbe hivyo mpaka pale daktari akivigundua wakati atakapofanya vipimo. Kwa upande mwingine, kama una vivimbe vingi, au kama ni vikubwa, basi vinaweza kusababisha dalili nyingi.  
 



FIBROID NI NINI?

Siku hizi kuna ongezeko kubwa sana la huu ugonjwa hebu tega sikio.
Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.


Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.

Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.



SABABU ZA MWANAMKE KUPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI

Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;

1. đź“ŽKuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini.
2.đź“Ž Ujauzito.
3.đź“Ž Uzito/ unene kupita kiasi.
4.đź“Ž Jenetiki zisizo za kawaida.
5.đź“Ž Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu.
6.đź“Ž Sababu za kurithi.
7.đź“Ž Lishe isiyo sawa/Lishe duni.
8.đź“ŽSumu na taka mbalimbali mwilini.


AINA ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI
Kuna aina kuu 3 za uvimbe kwenye kizazi kama ifuatavyo:

1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi)

2.Intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi)

3.Subserosal(nje ya kizazi)

WAFUATAO WAPO HATARINI KUPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI(UTERINE FIBROID)
1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa
2.miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma
3.kurithi
4.Unene/uzito kupita kiasi
5.kuingia hedhi mapema

Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto.
Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma.


DALILI ZA MWANAMKE MWENYE UVIMBE KWENYE KIZAZI (UTERINE FIBROIDS):

1.đź–‡️Kupata damu nyingi wakati wa hedhi.
2. đź–‡️Maumivu makali wakati wa siku za hedhi.
3. đź–‡️Kuvimba miguu.
4. Unaweza kuhisi una ujauzito.
5. đź–‡️Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
6. đź–‡️Kuhisi kuvimbiwa.
7. đź–‡️Kupata haja ndogo kwa taabu.
8. đź–‡️Kutokwa na uchafu ukeni.
9.đź–‡️ Kupata choo kigumu au kufunga choo.
10.đź–‡️ Maumivu nyuma ya mgongo.
11. đź–‡️Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto.
12.đź–‡️ Upungufu wa damu.
13.đź–‡️ Maumivu ya kichwa.
14.đź–‡️ Uzazi wa shida.
15.đź–‡️ Kutopata ujauzito.
16.đź–‡️ Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo.
17.đź–‡️ Maumivu ya nyonga.
18.đź–‡️ Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage).
19.đź–‡️ Kukojoa mara kwa mara kwan uvimbe huweka mgandamizo katika kibofu cha mkojo
20.đź–‡️ Hedhi zisizokuwa na mpangilio

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUPONA HARAKA UVIMBE KWENYE KIZAZI

1. đź“ŽHakikisha una uzito sawa kila mara kulingana na urefu wako.
2. đź“ŽKula sana mboga za kijani na matunda
3. đź“ŽFanya mazoezi ya viungo kila mara, mara 4 mapaka 5 kwa wiki
4. đź“ŽKunywa maji mengi kila siku lita mbili mpaka lita tatu
5. đź“ŽKula sana vyakula vyenye nyuzi nyuzi (faiba) na punguza vyakula vyenye mafuta
6. đź“ŽUsitumie bidhaa zozote zenye kaffeina (chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote nk), nyama nyekundu na vyakula vya kuchomwa au kupikwa katikati ya mafuta mengi (maandazi, chipsi, nk)
7. đź“ŽAchana kabisa na mawazo mawazo (stress) na hamaki nyingine zozote
8. đź“ŽAcha kuvuta sigara/tumbaku na vilevi vingine vyote hadi hapo utakapopona kabisa


MATIBABU/TIBA ASILI KWA UVIMBE KWENYE KIZAZI.

Tiba asili ndio njia salama na rahisi katika matibabu ya uvimbe kwenye kizazi endapo mgonjwa atafuata ushauri na matumizi sahihihi ya dawa.

Zipo dawa asili zenye ufanisi mkubwa sana katika kutibu uvimbe kwenye kizazi, Mfano ni dawa hizo ni FIBROCYST SOLUTION nk hii ni dawa yenye uwezo mkubwa sana katika kutibu uvimbe kwenye kizazi.







DALILI ZA VIUMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI (OVARIAN CYSTS) 
 
Vivimbe kwenye vifuko vya mayai hutofautiana ukubwa wake, lakini mara nyingi huwa ni nusu inchi hadi inchi 4 au vinawenaweza kuwa vikubwa zaidi na vinaweza kusababisha: 
 


• Maumivu kupenya kwenye tumbo la chini, mara nyingi sehemu moja 
• Tumbo la chini kuwa kubwa 
• Maumivu kiunoni au kwenye mapaja 
• Maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa 
• Maumivu wakati wa hedhi 
• Matiti kuuma 
• Kuhisi kukojoa mara kwa mara au hata huna mkojo 
• Kutokwa na damu ukeni isiyo ya kawaida 
• Matatizo katika njia ya haja kubwa 
• Uzito wa mwili kuwa mkubwa 
 
Uvimbe kwenye kifuko cha mayai unaweza kupasuka au kusababisha kifuko kujisokota kwenye umbo lake na kupelekea: 
 
• Maumivu makali ya ghafla tumboni 
• Homa au kutapika 
• Kuhisi kizunguzungu au kuzimia 
• Kupumua haraka haraka 
• Kutokwa na damu nyingi ya hedhi.

NUKUU: Vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) vinaweza kusababisha maumivu ya nyonga pamoja na tumbo la chini kuwa kubwa. Dalili mbili muhimu zinaweza kutoa ishara za aina moja ya uvimbe unaweza kuwa nao. Kwanza kabisa, maumivu kwenye tumbo la chini upande mmoja tu unaweza kusababishwa na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) kuliko vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids). Badala yake, kuwa na matatizo ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi inaweza kutokana na vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) kuliko vivimbe kwenye mayai(ovarian cysts).  
 
Dalili nyingi hizi zinaweza kutokana na matatizo mengine ya kiafya pia. Hii ndio maana unapofika hospitali kuonana na daktari ili kujua nini kinasababisha, ni jambo jema mno kuliko kukaa na tatizo muda mrefu.

Je, Vipimo Vya Vivimbe Kwenye Tumbo La Uzazi Au Kwenye Vifuko Vya Mayai Vinakuwaje? 
 
Daktari anaweza kuhisi kuwa una uvimbe kwenye tumbo la uzazi au kwenye vifuko vya mayai kulingana na dalili zako pamoja na vipimo kwenye nyonga. Vipimo fulani vya kuzamisha vinaweza kutoa taarifa zaidi, endapo kama tumbo la chini linakuwa kubwa na hasa popote uvimbe ulipo. Vipimo hivi vinaweza kuwa kama hivi vifuatavyo: 
 
• Kipimo cha kupima tumbo la chini(Abdominal Ultrasound) 
• Kipimo cha kuzamisha ukeni(Transvaginal Ultrasound) 
• MRI 
 
Kama vivimbe hivi vikiwa ndani au juu ukuta wa tumbo la uzazi, vinaweza kuwa ni fibroid, ambavyo pia huitwa, “myomas au leiomyomas.” 
 
Kama kuna uvimbe kwenye kwenye vifuko vya mayai, inaweza kuwa ni uvimbe maji. Kipimo cha ultrasound kinachozamishwa ukeni kinaweza kusaidia kubaini kama uvimbe ni mgumu au umejaa majimaji.






Je, Tiba Zake Zinakuwaje? 
  
Liwaya Herbal Clinic tuna tiba nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo ya vivimbe katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kutumia Dawa Asilia zinazotokana na Miti dawa FIBROCYST SOLUTION, UROGETIX 5,  THE HORMONE NA UZAZI CHANGO POWDER.

WASILIANA NA MIMI KWA USHAURI NA MATIBABU

DR LIWAYA

+255755162724

NAPATIKANA DAR ES SAALAM, ILALA

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...