Skip to main content

BAWASIRI,AINA ZAKE,DALILI ZAKE,AINA ZAKE,CHANZO CHAKE NA TIBA ASILI (KUOTA KINYAMA,MIWASHO ,DAMU SEHEMU YA HAJA KUBWA)

BAWASIRI,AINA ZAKE,DALILI ZAKE,AINA ZAKE,CHANZO CHAKE NA TIBA ASILI (KUOTA KINYAMA,MIWASHO ,DAMU SEHEMU YA HAJA KUBWA)

DAWA YA BAWASIRI
                  

Dr.Liwaya
+255755162724
liwayaherbal@gmail.com


BAWASIRI NI NINI?

-Bawasiri ni Ugonjwa unaotokana na kuvimba/kupasuka kwa mishipa ya dawa sehemu ya haja kubwa na kupelekea kuota kwa kinyama/Uvimbe ambao ndio huitwa Bawasiri.


Sababu kubwa ya mtu kupata Bawasiri ni Mgandamizo sehemu ya haja kubwa ambapo mgandamizo huo hupelekea kupasuka/kuvimba kwa mishipa midogo midogo ya damu aina ya veins sehemu ya haja kubwa hivyo hupelekea kuota kwa kinyama,miwasho,maumivu makali na kutoa damu

 Ugonjwa huu umekuwa ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.



   DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI

1.đź“Žkupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa
2.đź“Žkujitokeza kwa kinyama/vinyama eneo la haja kubwa
3.đź“Žkutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa
4.đź“Žkupata kinyesi chenye damu
5.đź“Žkupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
6.đź“Ž Kupata maumivu ya tumbo/kiuno hasa Bawasiri inapofikia hatua mbaya



AINA ZA BAWASIRI⤵️

-Kuna aina 2 za Bawasiri kama ifuatavyo⤵⤵⤵⤵:

1⃣. BAWASIRI YA NJE
Ni kuota kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa ambapo kinyama huwa nje hata kama hujaenda kujisaidia haja kubwa.

2.BAWASIRI YA NDANI
Ni kuota kinyama sehemu ya ndani ya haja kubwa mara nyingi huambatana na maumivu makali na damu na kinyama hutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.



Bawasiri ya ndan ina hatua NNE ambazo ni:⤵⤵⤵⤵:

1. HATUA YA KWANZA

Katika hatua hii mtu hujihisi maumivu makali,miwasho pamoja na kutokwa damu wakati wa kujisaidia na kinyama hakionekan wakati wa kujisaidia.

2. HATUA YA PILI 

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe punde baada ya kujisaidia

3.HATUA YA TATU 

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe ama inaweza kurud yenyewe baada ya muda 

4. HATUA YA NNE

Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi baada ya kujisaidia.



VISABABISHI/MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI

1.đź–‡️ Uzito kupita kiasi(Overweight)
2.đź–‡️ Ujauzito
3.đź–‡️ Unywaji pombe
4.đź–‡️ Kukaa sana sehemu ngumu
5.đź–‡️ Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa.
6.đź–‡️Kujisaidia Choo Kigumu.Sababu za kujisaidia choo Kigumu ni:
-Vidonda vya TUMBO
-Ngiri/Hernia
-Ulaji duni
-Kuwa na acid mwingi tumboni

7.đź–‡️ Kula sana nyama nyekundu
8.đź–‡️ Presha ya kupanda
9.đź–‡️ Kula sana pilipili
10.đź–‡️ Kula udongo(Wajawazito na watoto wadogo)
11.đź–‡️ Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa
12.đź–‡️ Kuharisha kupita kiasi.
13.đź–‡️ Kufanyakaz ngumu/kunyanyua vitu vizito



MADHARA/ATHARI ZA BAWASIRI

1.đź“ŽUpungufu wa damu mwilini
2.đź“ŽKutokwa na kinyesi bila kujitambua 
3.đź“Žkukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
4.đź“Žkupungukiwa nguvu za kiume
5.đź“Žkupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
6.đź“ŽKupata tatizo la kisaikolojia 
7.đź“ŽKutopata ujauzito
8.đź“Ž Mimba kuharibika
10.đź“Ž Kupata kansa ya utumbo ( Colorectal cancer)
11.đź“Ž Mwili kudhoofika



NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI

1.đź“ŽKula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi 
2.đź“Žkunywa maji mengi lita 2.5 hadi 3 kwa siku
3.đź“ŽAcha kufanya mapenzi kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
4.đź“ŽPunguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.
5.đź“Ž Acha kunywa pombe
6.đź“ŽPunguza kula nyama nyekundu
7.đź“ŽPunguza matumizi ya pili pili.
8.đź“ŽJitibie vidonda vya tumbo
9.đź“Ž Jitibie Ngiri
10.đź“Ž Dhibiti uzito wako
11.đź“Ž Jiepushe/punguza kunyanyua vitu vizito mara kwa mara



MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI

Kuna matibabu aina mbili katika kutibu ugonjwa wa Bawasiri:

1.đź“Ž MATIBABU YA KISASA

-Matibabu ya kisasa yanahusisha matibabu ya Hospital ambapo tiba kubwa ya Bawasiri kwa hospital ni kufanyiwa upasuaji mdogo ( minor surgery) kwaajili ya kuondoa kinyama. Changamoto kubwa ya matibabu haya ni kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanya upasuaj wa tatzo hili tatizo hujirudia kwasababu upasuaji huondoa athari ya tatzo na si mzizi wa tatizo yaani ni sawa na kukata mti kisha ukaacha mizizi bila shaka mti huo utachipua na kumea tena.Lakini pia Upasuaji wa Bawasiri huwa na maumivu makali sana na uponaji wa kidonda hufika mpaka miezi miwili,hali hii ya kukaa na kidonda kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata Kansa ya utumbo ( Colorectal Cancer).



2.đź“Ž MATIBABU KWA NJIA ASILI

-Matibabu haya yanahusisha utumiaji wa dawa zinazotokana na mimea dawa.Dawa hizi Hutibu Bawasiri bila kufanya upasuaji na huweza kuleta matokeo ya haraka kwa mgonjwa endapo atatumia dawa huku akijitahid kujiepusha na visababishi vyote vinavyopelekea mtu kupata Bawasiri. Zipo dawa asili nyingi na nzur sana katika kutibu Bawasiri, mfano wa dawa hizo ni Bawasiri Fluid na Bawasiri powder,dawa hizi zina ufanisi mkubwa katika kutibu Bawasiri endapo Mgonjwa atazingatia maelekezo.



ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAGONJWA WENGI WA BAWASIRI KUTUMIA DAWA NYINGI BILA MAFANIKIO

Kwanza Mgonjwa wa Bawasiri anatakiwa kufahamu ya kwamba,matibabu si dawa pekee.Watu wengi wanaamin kwamba matibabu ni dawa pekee na jambo hili limepelekea wengi kuteseka na matatzo kwa muda mrefu sana bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa ya kutafuta tiba na badala yake humuona kila mtoa huduma ni tapeli:

Zifuatazo ni sababu zinazowafanya wagonjwa wengi kuteseka na Bawasiri kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa mbali mbali:



1.đź“Ž Kutopata dawa sahihi 

-Si kila dawa inayotangazwa kutibu Bawasiri inaweza kutibu Bawasiri bali dawa yenye ufanisi wa kutibu ndio inaweza kutibu Bawasiri.



2.đź“Ž Kutofuata ushaur wa daktari.

-Usipofuata yale ambayo daktari anakuelekeza ili kupata suluhisho la Tatzo lako ni ngumu kupona tatzo lako.



3.đź“Ž Kutoziacha sababu zilizopelekea upate Bawasiri. Katika hili wengi wamefeli kwani haiwezekani ukapona Bawasiri ikiwa sababu zilizopelekea upate Bawasiri hutaki kuziacha mfano;

-Pombe
-Uzito mkubwa
-Ulaji mbovu
-Kuingiliwa kinyume 
-Kula sana pilipili
-Kukaa sana sehemu ngumu.
-Kunyanyua vitu vizito
-Kutotibu Magonjwa kama Ngiri na Vidonda vya TUMBO
-Kutokula vyakula vya kulainisha choo kama vile Mboga za majani & matunda
-Kula udongo(wajawazito)
-Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa.
-Kuharisha mara kwa mara
-Kujisaidia choo Kigumu



Hata utumie dawa zaid ya 100,usipoziacha sababu hizo ni ngumu sana kupona Bawasiri na matokea yake kila mtoa tiba utamuona Tapeli kumbe sababu ni wewe mwenyewe kutofuata miongozo,maelekezo na USHAURI kutoka kwa daktar.



⚫ Ukizingatia hayo utapona Bawasiri kwa muda mfupi sana(week 1 mpaka 3) Biidhnillaah japo wapo wanaopona kwa siku 5 licha ya kukaa na Bawasiri kwa miaka kadhaa .


Dr.Liwaya
+255755162724
liwayaherbal@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...