Skip to main content

DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

Ujauzito huja na tabia nyingi ambazo baadhi huwa za kawaida huku baadhi zikiwa siyo za kawaida.

Ni muhimu sana kwa mama mjamzito kuzungumza na daktari mara kwa mara ili kuondoa sintofahamu hizi ambazo siyo nzuri kwa afya.




Tumekuletea dalili za hatari wakati wa ujauzito ambazo ni lazima zishughulikiwe haraka ili kuzuia madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa mama na mtoto.

1. Damu kwenye via vya uzazi
Katika mazingira ya kawaida, damu huwa haipaswi kutoka wakati wote wa ujauzito.

Katika mazingira fulani, siku ya 10-14 baada ya kutungwa kwa ujauzito mwanamke anaweza kutokwa na damu kidogo ambayo humaanisha kuwa kijusi kinajishikiza kwenye mji wa uzazi ili kianze kulelewa.

Kutokwa na damu kwenye via vya uzazi muda wowote mwingine siyo ishara nzuri hivyo inapawa kuchukuliwa kama jambo la dharura.

Baadhi ya sababu zinazoweza kufanya damu itoke ni uwepo wa maambukizi makubwa, tishio la kuharibika kwa ujauzito, kuwa na ujauzito unaolelewa nje ya mji wa uzazi au uwepo wa changamoto zozote kwenye kondo la uzazi.

2. Kifafa na degedege
Shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito ambalo huambatana na uwepo wa protini kwenye mkojo husababisha kifafa cha ujauzito.

Hali hii ya kifafa na degedege huwa ni hatari kwa afya ya mama na mtoto.

Inaweza kusababisha kifo cha mama au mtoto, kuharibika kwa ujauzito, kujifungua kabla ya wakati, kuathiri mfumo wa fahamu, kuharibu viungo vya mwili, upofu pamoja na kujifungua watoto wenye tatizo la degedege.

3. Kichwa na macho
Maumivu makali ya kichwa na kupungua uwezo wa macho kwenye kuona ni dalili za kifafa cha ujauzito.

Ni muhimu sana kwa mwanamke mjamzito kufika hospitalini haraka.

Dalili hizi mara nyingi huonekana kuanzia wiki ya 20 ya ujauzito na kuendelea.

4. Mtoto kuacha kucheza
Baadhi ya watoto huanza kucheza kuanzia wiki ya 13-16 tangu mwanamke aone hedhi yake ya mwisho.

Kwa wanawake wenye ujauzito wa kwanza wanaweza kuchelewa hadi wiki ya 18-20 ndipo wahisi miondoko ya mtoto.

Kwa kuwa kila mwanamke hupata ujauzito kwa namna yake, wastani wa muda wa kawaida wa kuanza kucheza kwa mtoto huwa ni kuanzia wiki ya 13-25.

Kama mtoto alikuwa kazoea kucheza kisha akaacha ghalfa, unapaswa kuwa na wasiwasi maana hii siyo ishara nzuri.

Fika hospitalini kwa uchunguzi ili kufahamu kama tukio hili lina maana nzuri au mbaya.

5. Maumivu makali tumboni
Maumivu makali ya tumbo hasa yale yanayotokea kwenye sehemu ya chini ya tumbo huwa siyo mazuri.

Maumivu haya yanaweza kuambatana na hali ya kukaza kwa misuli ya tumbo.

Yanaweza kuwa na maana kuwa mwanamke anataka kupatwa na uchungu wa mapema kabla ya muda halisi.

Ni muhimu kufika hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.

6. Kupasuka kwa chupa
Mtoto huhifadhiwa kwenye nyumba ya uzazi ambayo kwa lugha rahisi inayofahamika zaidi huitwa chupa ya uzazi.

Chupa hii haipaswi kupasuka muda wowote ule kabla ya uchungu wa kuzaa.

Wastani wa asilimia 3-10 ya wanawake wote wanaojifungua.

Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya siku sahihi ya uchungu husababisha maambukizi kwa mama na mtoto, kunyofoka kwa kondo la uzazi pamoja na changamoto kwenye kitovu.

Ni muhimu kufika hospitalini ili tiba sahihi iweze kutolewa.

Inaweza kuhusisha matumizi ya dawa, sindano au kuzalishwa haraka ikiwa ujauzito utakuwa umefikia kwenye hatua ambayo mtoto akitolewa ataweza kuishi.

7. Homa kali
Kupanda kwa joto hadi 100.4°F (38°C) siyo jambo zuri kutokea wakati wa ujauzito.

Homa hii inaweza kuwa hatari zaidi kama itaambatana na kiungulia, kuhara, maumivu makali ya tumbo na mgongo, kupungua kwa mkojo pamoja na kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi na hatufu kali.

Inaweza kuwa ishara ya uwepo wa maambukizi makali kwenye sehemu mbalimbali za mwili hasa zile zinazohusisha figo, mji wa uzazi au mapafu.

8. Maumivu ya kifua
Katika mazingira ya kawaida, maumivu ya kifua wakati wa ujauzito huwa hayana maana mbaya.

Husababishwa na kiungulia, au mgandamizo mkubwa unaofanywa na mtoto kwenye kusukuma viungo vya mwili kuelekea nafasi ya wazi ya kifua.

Hali inaweza isiwe ya kawaida kama maumivu haya ya kufua yataambatana na changamoto za kupumua pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo.

Uchunguzi wa haraka unahitajika.

9. Uvimbe
Kuvimba kwa mwili wakati wa ujauzito (Edema) ni jambo linalotokea kwa wanawake wengi. Uvimbe huu mara nyingi hutokea kwenye mikono, miguu, uso na maungio ya mifupa.

Hata hivyo, katika nyakati chache, kuvimba kwa mwili kunaweza kuwa dalili mbaya ya uwepo wa changamoto kubwa za kiafya hasa shinikizo kubwa la damu linaloweza kuleta kifafa cha mimba pamoja na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu maarufu zaidi kama deep vein thrombosis (DVT) ambayo ni chanzo cha kiharusi.

Ni muhimu kufika hospitalini haraka kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Ikiwa ujauzito hauna tishio lolote la kuharibika, njia nzuri na rahisi ya kuzuia tatizo la kuvimba kwa mwili ni kushiriki mazoezi mepesi hasa yale ya kutembea, kufanya kazi ndogondogo za nyumbani pamoja na kuacha tabia ya kukaa (kupumzika) muda mrefu pasipo kujishughulisha na jambo lolote.


Naomba niishie hapa. Nikaribishe Maswali, Karibuni Sana..



Je, Unahitaji Kupata Huduma Kutoka Liwaya Herbal Clinic ? Basi wasiliana nasi Kwa namba hizi: 0755162724



Pia Unaweza kutembelea tovuti yetu: www.liwayaherbalclinic.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...