UGONJWA WA UTI CHANZO, DALILI, NAMNA YA KUJIKINGA NA TIBA YAKE ASILIA
Kuelewa vizuri tunachokizungumzia hapa, tazama picha ya viungo hivi na kwa kifupi hapa tutatoa maelezo ya picha hiyo. Figo ni viungo viwili vilivyopo kimoja kila upande wa uti wa mgongo eneo la kiunoni. Figo hufanya shughuli nyingi katika mwili wa binadamu ikiwepo ya kutoa uchafu na maji ya ziada katika damu, na huvitoa vitu hivi kama mkojo. Kwa sababu hii, figo ni muhimu sana katika kuweka msukumo wa damu kwenye kiwango kizuri. Figo pia husikia mapema sana mabadiliko ya kiwango cha sukari mwilini na mabadiliko katika kiwango cha msukumo wa damu (blood pressure). Kiwango cha sukari na msukumo wa damu vikizidi, vyote huweza kuleta madhara kwenye figo.
SABABU ZA UGONJWA WA UTI
Ureters ni mirija miwili myembamba yenye urefu wa yapata nchi 10 hivi kila mmoja ambayo huchukua mkojo kutoka kwenye figo na kuumwaga ndani ya kibofu cha mkojo.
Kibofu cha mkojo ni kijimfuko kidogo kinachopokea mkojo kutoka kwenye mirija ya ureters na kuuhifadhi. Mkojo ukifikia kiwango fulani ndani ya kibofu cha mkojo, tunasikia haja ya kuupunguza (kukojoa) na ndipo misuli ya nje ya kibofu cha mkojo hujibana na kuukamua mkojo nje ya kibofu.
Urethra ni mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na nje ya mwili.
Sehemu yo yote katika hizi tulizozitaja hapa juu, inaweza ikapata maambukizi ya UTI na kadri maambukizi hayo yatakavyokuwa ndani zaidi ukitokea nje, ndivyo ugonjwa huu utakavyokuwa umefikia hali mbaya zaidi. Wasichana na akina mama hupata maambukizi haya kwa wingi zaidi kuliko wavulana au akina baba. Asilimia kama 40 ya wanawake na asilimia 12 ya wanaume hupata maambukizi haya ya UTI katika maisha yao.
DALILI ZA UGONJWA WA UTI
-Dalili za ugonjwa huu ni kama zifuatazo
- đź”´Maumivu wakati wa kukojoa - (mkojo kuunguza unapotoka – burning with urination).
- đź”´Kukojoa mara kwa mara (kidogo kidogo).
- đź”´Kujisikia haja ya kukojoa wakati kiuhalisia kibofu hakuna mkojo.
- đź”´Homa, kutapika, kichwa kuuma huweza kuambatana na dalili hizo
- đź”´Maumivu ya kiuno, Na mgongo wa chini – lower back pain
- đź”´Mkojo wenye damu (mara chache hutokea), wakati mwingine usaha kwenye mkojo
- Kwa wazee na watoto wachanga dalili za UTI huweza kutatiza kuzijua(vague symptoms)
- Watoto – kushindwa kuzuia mkojo – kujikojolea huweza kuwa dalili y maambuki ya uti
- Mkojo kwa kawaida ni kitu kisicho na wadudu wo wote wabaya. Maambukizi yanakuja pale wadudu wanapoingia kwenye mkondo wa mkojo kupitia kitundu cha kutolea mkojo nje ya mwili na kufuata mkondo huo kuelekea kwenye figo. Wadudu hao wakishaingia huanza kuzaliana. Asilimai 90 ya maambukizi yasiyo mabaya sana huwa ni ya bacteria waitwao Escherichia Coli au kwa kifupi E. Coli. Kwa kawaida bacteria hawa huishi katika utumbo au karibu na maeneo ya mkundu. Wadudu hawa wanaweza wakatembea kutoka eneo la mkundu wakaelekea kwenye tundu la mkojo na kuingia. Lakini, kutojisafisha kwa namna nzuri (kwa mfano, kutawadha kuanzia nyuma kuja mbele) au ngono ndizo njia mbazo huambukiza bacteria hawa kirahisi zaidi.
- Sababu zinazoweza kuchochea (risk factors) ni pamoja na maumbile ya kike (female anatomy), kujamiiana (sexual intercourse), unene uliopitiliza(obesity), historia katika familia.
- -Wanawake hupatwa zaidi na maambukizi haya kwa sababu ya ukaribu wa mkundu na kijitundu cha kutolea mkojo na kwa sababu ya ufupi kati ya urethra na kibofu cha mkojo katika miili yao ukilinganisha na wanaume. Wanawake wanaoshiriki ngono mara nyingi na watu tofauti hupatwa na maambukizi zaidi kuliko wale wanaoshiriki kwa kiwango kidogo.
- Wanawake wanaotumia diaphragms kama njia ya uzazi wa mpango hupatwa zaidi na tatizo hili pia akina mama waliokoma hedhi kwa sababu ya ukosefu wa homoni ya estrogen. Kukosekana kwa estrogen kunasababisha mabadiliko katika mkondo wa mkojo na kuufanya uweze kuambukizwa kwa urahisi zaidi.
- Matatizo yo yote yanayosababisha mkojo usitoke nje kwa urahisi huongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UTI. Mifano ni; watoto kuzaliwa na matatizo katika mikondo yao ya mkojo ambayo huzuia mkojo usitoke nje kirahisi, matatizo ya kidney stones na prostate kukua kupita kiasi; na watu wanaotoa mkojo kupitia kifaa maalumu (catheter).
- Tendo la kukojoa huwatoa bacteria hawa nje ya mwili lakini wakiwa wengi sana, kukojoa hakuwezi kuwatoa wakaisha. Wadudu hawa husafiri kwenye urethra hadi kwenye kibofu cha mkojo ambako watazaliana. Wanaweza kuendelea kusafiri kupitia ureters hadi kwenye figo ambako pia watazaliana na kuleta matatizo makubwa endapo tiba nzuri haitatolewa kwa wakati muafaka.
- ⚫Ikumbukwe – uti sio ugonjwa wa zinaa hivyo usije ukamlaumu mwenzi wako kwamba ana UTI hivyo amechepuka, la hasha! ugonjwa huu zamani ulijulikana kama honey moon cystitis – maana uliwapata zaidi wenzi waliotoka kufunga ndoa sababu ilihusishwa na hali ya kukutana kimwili hasa wanapokuwa fungate.
- ⚫Wakati mwingine UTI husababishwa na maambukizi ndani ya damu (Blood borne) na husambaa hadi kwenye figo na kuleta UTI.
- ⚫Vilevile kwa wagonjwa waliowekewa mpira wa mkojo – catheter huwa chanzo cha bakteria waletao UTI.
- Kujamiiana – sexual intercourse – zaidi ya asilimia 75 – 90 ya wanawake wanaoshiriki sex hupatwa na UTI, na uwezekano wa kupata huongezeka zaidi kulingana na ufanywaji wa tendo mara kwa mara. (Kama nilivyoeleza juu ya honeymoon cystitis)
JINSI YA KUGUNDUA – DIAGNOSIS
Daktari atakuomba ulete mkojo ili upimwe katika maabara – urinalysis pamoja na urine microscopy. Pia kuoteshwa mkojo – urine culture – ili kugundua aina wa bakteria walioshambulia mfumo wa mkojo.
Aina za UTI zinazoonekana zaidi ni zile ambazo huwashambulia wanawake na hushambulia kibofu cha mkojo na urethra.
đź”´Maambukizi ya kibofu cha mkojo (cystitis). Aina hii ya UTI mara nyingi huhusisha bakteria aitwaye Escherichia coli (E.coli), aina ya bakteria anayepatikana ndani ya mkondo wa mmeng’enyo wa chakula (gastrointestinal tract – GI). Lakini, mara nyingine aina nyingine za bakteria wanaweza kuhusika.
Tendo la ndoa linaweza kusababisha cystitis, na si lazima ushiriki ngono sana kuweza kuupata ugonjwa huu. Wanawake wote wapo hatarini kuupata sababu ya maumbile yao – ikiwa ni ukaribu wa urethra na tundu la haja kubwa na ule wa urethra na tundu la kibofu cha mkojo.
Maambukizi ya urethra (urethritis). Aina hii ya UTI huweza kutokea pale bakteria kutoka kwenye mkondo wa chakula wanapoweza kusambaa kutoka kwenye mkundu hadi kwenye urethra. Na, kwa sababu urethra ya mwanamke ipo karibu na uke wa mwanamke, magonjwa ya ngono kama herpes, gonorrhea, chlamydia na mycoplasma, yanaweza kusababisha urethritis.
NI ZIPI DALILI ZA UGONJWA WA UTI?
Dalili za ugonjwa huu huwa tofauti kulingana na hatua ambayo ugonjwa umeshafikia.
Lower UTI ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, mgonjwa atasikia dalili zifuatazo:
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu
- Damu katika mkojo
- Mkojo wenye rangi ya chai
- Mkojo wenye harufu kali
- Maumivu ya kiuno kwa wanawake
- Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume
Upper UTI ni maambukizi ya ndani ya figo. Hii ni hatua mbaya sana endapo bacteria wataanza kuingia kwenye mkondo wa damu kutoka kwenye figo – SEPSIS. Sepsis huweza kusababisha msukumo wa damu kuwa mdogo sana (Low Blood Pressure), mshituko au kifo.
Dalili za upper UTI ni:
- Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo
- Homa
- Kusikia baridi
- Kusikia kichefuchefu
- Kutapika
JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA UTI
- Kunywa maji ya kutosha na vimiminika vingine kama juisi za matunda, miwa, maji ya madafu – hii husaidia kuondoa vimelea vinavyoanza kuota na kutanda katika kuta za mfumo wa mkojo. Usipokunywa maji ya kutosha angalau lita 2 na nusu kwa siku kwa mtu mzima UTI itakusumbua.
- Epuka matumizi ya vyoo vinavyotumika na watu wengi, au hakikisha usafi wake, kabla na baada ya kutumia. – vyoo vinapotumika na watu wengi na hasa vya kukaa au kuchuchumaa huweza kuwa chanzo cha UTI, maana katika watu wengi wamo walio na maambukizi katika mkojo huacha bakteria na kuenea kwa wengine watakaotumia choo hicho. Inapobidi kutumia hicho, safisha kwa maji mengi na sabuni ndipo utumie.
- Kukojoa kwa haraka mara umalizapo tendo la kujamiiana – hii husaidia kusafisha njia ya mkojo na kuzuia wadudu kudanda katik kuta za mfumo wa mkojo na kuleta madhara. Kojoa haraka na kuwaondoa bakteria wale amabao kwa bahati mbaya waliingia wakati wa tendo la sex
- Kubadilisha aina ya nguo za ndani – kama unapata UTI Zaid ya mara tano kwa mwaka, chunguza nguo za ndani na pata ushauri wa wataalamu ubadilishe kuepuka UTI Marakwa mara pia ni bora kuvaa chupi zilizo tengenezwa kwa pamba
- Usafi binafsi wakati wa kwenda haja ndogo na wakati wa haja kubwa
- Usafi wa bafuni
- Usichelewe kwenda kukojoa kwa kushukili mkojo muda mrefu.
- Wenye tezi dume kukojoa wakiwa wamekaa hupunguza maambukizi.
Ni vema kwa wale wana ndoa wakapima mkojo kwa pamoja, hasa inapotokea mwanamke ana UTI ni vizur mwanaume na yeye apimwe na kupatiwa matibabu kusaidia mwanamke asipate maambukizi kwa kujirudia.
TIBA YA UGONJWA WA UTI
Zipo dawa mbalimbali za kuuwa bakteria zinazotibu Ugonjwa wa UTI. Miongoni mwa hizo kuna Dawa inaitwa UROGETIX 5 ni katika dawa zilizo gundulika kuwa na ufanisi mzuri katika kutibu Ugonjwa wa UTI
Lakini tiba ispotolewa kwa wakati, maambukizi haya ya mkondo wa mkojo huweza kuleta matatizo makubwa. Pamoja na mengineyo, mgonjwa anaweza:
- . Kupata maambukizi ya mara kwa mara
- . Kupata uharibifu wa figo wa kudumu na kuhitaji huduma maalumu ya kutibu figo (dialysis).
- . Kutokea uwezekano wa kuzaa watoto wenye uzito mdogo au wanaozaliwa kabla ya wakati.
- . Wanaume wanaougua UTI mara kwa mara wanakuwa kwenye hatari ya kupata madhara kwenye tezi dume (prostatitis).
- . Uvimbe huweza kutokea kwenye tezi dume na kusababisha maumivu wakati wa haja ndogo au kutoa shahawa.
- . Sumu katika damu. Mara chache huweza ikatokea kuwa bakteria wakasambaa kutoka ndani ya figo na kuingia kwenye mfumo wa damu (sepsis) na baadaye kusambaa hadi kwenye viungo vingine muhimu vya mwili. Hali hii ikitokea, itabidi mgonjwa awekwe chini ya uangalizi mkali wakati akipewa tiba ya kuwaua bakteria hao.
Usisite kuuliza swali au kutoa maoni yako kuhusiana na mada yetu. Tutafurahi sana kusikia kutoka kwako na kukujibu.
Unaweza kuwasiliana nasi kwa msaada wa kimatibabu na ushauri kiujumla kuhusiana na matatizo mbalimbali ya kiafya
Kwa maelezo zaidi na ya kina, tuma ujumbe wako sms/WhatsApp kupitia namba hizi +255755162724
Tupo Dar es salaam, Ilala mtaa wa Pangani na Utete, Nyumba namba 18, Ground Floor.
Chukua hatua, mwambie na mwenzio UTI ni Ugonjwa hatari.
Asanteni.
Comments