Skip to main content

TATIZO LA KUFUNGA CHOO NA KUPATA CHOO KIGUMU

Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili.


Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3.

Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu. Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka. Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku. Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku.

Inatakiwa ifahamike kuwa kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea mtu kupata choo kigumu au kufunga choo. Miongoni mwa sababu hizo ni ni kuwa na baadhi ya magonjwa kama Vidonda vya tumbo, Kuzidi kwa Acid tumboni na Ugonjwa wa Ngiri (Hernia).

Ikiwa sababu ya kupata choo kigumu au kukosa kabisa choo inatokana na hayo maradhi ya Vidonda vya tumbo, Kuzidi kwa Acid tumboni na Ngiri una shauriwa kujitibia hayo magonjwa, ni ngumu kupona tatizo la choo ikiwa bado una moja katika hizo changamoto

DAWA MBADALA 10 ZINAZOTIBU KUFUNGA CHOO AU CHOO KIGUMU:

1. MAFUTA YA ZEITUNI (olive oil)


Mafuta ya zeituni (olive oil) yanatosha kutibu hili tatizo.
Yana radha nzuri mdomoni na ni dawa pia. Kama unaweza yafanye pia kama mafuta yako ya kupikia vyakula vyako mbalimbali, mafuta haya huweza kuliwa pia bila kupitishwa kwenye moto na hivyo ni mafuta mazuri kuweka kwenye kachumbari au saladi mbalimabali.

Matumizi: Chukua kijiko kikubwa kimoja cha mafuta ya zeituni changanya na kijiko kidogo kimoja cha chai cha maji maji ya limau na unywe asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa bado tupu. Fanya hivi kila siku mpaka utakapopona.

2. JUISI YA LIMAU



Juisi ya limau inatumika kutibu tatizo la kupata choo kigumu au kufunga choo.
Chukua maji maji ya limau kutoka katika limau kubwa 3 na uchanganye na juisi ya matunda kupata kikombe kimoja (ml 250) na unywe yote kutwa mara 1 kila siku kwa siku kadhaa mpaka umepona. Ukiacha hilo la kutibu kufunga choo limau ina vitamini C nyingi na hivyo itakuongezea kinga yako ya mwili kwa haraka zaidi (usizidishe hata hivyo).

3. MAZOEZI YA KUTEMBEA


Kama unataka kupata choo kilaini na cha kawaida basi jitahidi uwe mtu wa kutembeatembea na si kukaa tu kwenye kiti kutwa nzima. Maisha yetu ya kisasa na kazi za ofisini zinatulazimisha kuwa watu wa kukaa kwenye kiti masaa mengi wengine huamua tu kukaa kwenye kiti sebureni akiangalia TV asubuhi mpaka jioni!.

Aina hii ya maisha ni hatari zaidi kwa afya zetu kuliko hata madawa ya kulevya. Jitahidi kila siku uwe unapata muda wa kutembeatembea kwa miguu mpaka dakika 60 au zaidi. Hii itakusaidia kuondoa tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

4. VYAKULA VYA NYUZINYUZI (fiber)


Mara nyingi utasikia watu wakisisitiza juu ya umhimu wa kula vyakula vya asili na vyenye nyuzinyuzi. Chakula cha asili kina nafasi kubwa katika kuimarisha afya yako kwa ujumla. Kinachonishangaza ni kuona watu bado wanaendelea kula ugali wa sembe ilihali inajulikana wazi ugali mweupe ndiyo chanzo kikuu cha kupata choo kigumu ikiwemo ugonjwa wa bawasiri.

Ninakusihi sana uanze kula ugali wa dona kuanzia sasa na kuendelea. Hakikisha pia asilimia 80 ya mlo wako kwa siku ni matunda na mboga za majani. Matunda kama ndizi na parachichi ni mhimu ule kila siku kadharika tumia unga au mbegu za maboga.

5. MSHUBIRI (Aloe Vera)


Mshubiri unajulikana wazi kwa kutibu tatizo hili la kufunga choo au kupata choo kigumu. Ni mhimu utumie mshubiri fresh kabisa kutoka kwenye mmea moja kwa moja kuliko kutumia za dukani au za kwenye makopo. Usitumie zaidi ya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya shubiri kwa siku.

Matumizi: Changanya vijiko vikubwa viwili vya jeli ya aloe vera ndani ya kikombe kimoja cha juisi ya matunda uliyotengeneza mwenyewe nyumbani (hasa juisi ya parachichi) na unywe yote kutwa mara 1 hasa nyakati za usiku unapokaribia kwenda kulala kwa siku kadhaa au mpaka umepona.

6. BAKING SODA


Baking soda ni dawa nyingine ya asili nzuri kwa tatizo hili. Inafanya kazi vizuri kwa zaidi ya asilimia 95. Sababu ya bicarbonate iliyomo ndani yake itakusaidia kupumua nje vizuri gesi au hewa yoyote ilisongamana ndani ya tumbo pia inasaidia kupunguza asidi mwilini. Baking soda ni ile wamama huitumia katika kupika maandazi au mikate inapatikana katika maduka ya kawaida hata hapo nje kwa Mangi ipo.

Matumizi: -Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha baking soda ndani ya nusu kikombe cha maji ya uvuguvugu (ml 125) na unywe yote kwa haraka kutwa mara 1 kwa siku 7 hivi au unaweza kuacha siku yoyote kabla kama tatizo litakuwa limeisha.

7. MTINDI


Unahitaji bakteria wazuri zaidi wakati huu unapokabiliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Utahitaji pia kuacha kula vyakula vya kwenye makopo (processed sugars and foods). Namna rahisi kabisa ya kuhakikisha mwili wako unapata bakteria wazuri ni kwa kutumia mtindi. Tumia mtindi wowote ule uliotengeneza mwenyewe nyumbani au hata wa dukani (ila wa dukani usiwe umeongezwa vitu vingine ndani yake – sweetened yogurt).

Matumizi: Kunywa kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi wakati wa chakula cha asubuhi na kikombe kingine usiku unapoenda kulala kwa wiki 1 hata 2.

8. FANYA MAZOEZI YA KUSIMAMA NA KUCHUCHUMAA (squat)


Fanya mazoezi ya kuchuchumaaa na kusimama (squatting). Hili ni zoezi mhimu kwa mtu anayesumbuliwa na tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana. Fanya kuchuchumaa na kusimama mara 25 na upumzike dakika 1 kisha unaendelea tena unachuchumaa na kusimaa hivyo hivyo mara 25 kwa mizunguko mitano (5 rounds) huku ukipumzika dakika 1 kila baada ya mzunguko mmoja.

Fanya zoezi hili kila siku mara 1 na usizidishe sana, ni mara 25 kwa mizunguko mitano inatosha na uzuri ni kuwa unaweza kufanya zoezi hili mahali popote. Wakati huo huo unashauriwa kutumia choo cha kuchuchumaa yaani vile vyoo vya zamani na siyo hivi vya kisasa vya kukaa kama vile upo ofisini. Vyoo hivi vya kukaa ndiyo moja ya vitu vinavyochangia upate pia ugonjwa wa bawasiri (kuota kinyama sehemu ya haja kubwa na kupata maumivu wakati unajisaidia).

9. MATUNDA


Asilimia 80 ya chakula chacko kwa siku iwe ni matunda na mboga za majani. Unapoumwa na hili tatizo pendelea zaidi parachichi, papai na juisi ya ukwaju. Kula matunda siyo mpaka uumwe au ushauriwe na daktari, fanya kuwa ndiyo tabia yako kila siku na hutakawia kuona mabadiliko makubwa kwa afya yako kwa ujumla.

10. MAJI YA KUNYWA


Maji ni uhai Asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Asilimia 85 za ubongo wako ni maji. Asilimia 94 ya damu yako ni maji. Hakuna maisha bila maji. Inashangaza sana kuona mtu anamaliza siku nzima au hata siku 2 hajanywa maji! Kama wewe si mpenzi wa kunywa maji ya kutosha kila siku SAHAU KUWA NA AFYA NZURI MAISHANI MWAKO.

Hakikisha unakunywa maji kila siku lita 2 mpaka 3, kidogo kidogo kutwa nzima bila kusubiri kiu na hutaugua tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu. Dawa nyingine nzuri kwa ajili hii ni unga wa mbegu za mlonge

Kama umekuwa ukisumbuliwa na tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu unaweza kuwasiliana na mimi kwa ushauri na matibabu

Napatikana Dar es salaam, Ilala mtaa wa Pangani na Utete

Dr Liwaya
+255755162724

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...