Skip to main content

PID,SABABU ZAKE,DALILI ZAKE,KUJIKINGA KWAKE NA MATIBABU YAKE KWA DAWA ASILI

 PID SABABU ZAKE DALILI ZAKE KUJIKINGA KWAKE NA MATIBABU YAKE KWA DAWA ASILIA


    DAWA YA PID


Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari.


Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno.


 



PID MAENEO YA pid


Dalili Za PID

PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa:


. Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga

. Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya

. Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi

. Maumivu wakati wa kujamiiana

. Homa, wakati mwingine kusikia baridi

. Maumivu wakati wa haja ndogo, haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.


 


Chanzo Cha PID

Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.


 



PID kusambaa kwa PID


Aghalabu, bakteria hawa huingia kwenye viungo ya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa kwenye shingo ya kizazi (cervix) unapovurugwa. Hii inaweza kutokea mathalani, wakati wa hedhi na baada ya kuzaa, mimba kuharibika au kutoa mimba. Mara chache bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa cho chote cha tiba kinapoingizwa kwenye nyumba ya uzazi.


Mazingira Hatarishi

Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:


. Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono

. Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja

. Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja

. Kufanya mapenzi bila kinga

. Kujisafisha na maji mara kwa mara

. Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono


 


Madhara Yatokanayo Na PID

PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke. Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi.


 


 


PID magonjwa


Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na:

. Mimba nje ya mirija (ectopic pregnancy). PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi . Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.


. Ugumba. Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba – kushindwa kupata ujauzito. Kadiri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi, ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi. Kuchelewa kupata tiba ya PID kunaongeza hatari ya ugumba.


. Maumivu sugu ya nyonga. PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai linadodondoshwa (ovulation).


. Tubo-ovarian abscess. PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi. Mara nyingi majibu haya hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi. Kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizo hatarishi kwa maisha.


Tiba Ya PID

Tiba ya mara moja kwa kutumia dawa itaondoa maambukizo yaliyosababisha PID. Lakini, hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na PID. Tiba ya PID yaweza kuwa:


. Antibiotics. Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako. Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi.


. Kumtibu Mwezi wako. Kuzuia maambukizi, yafaa mwezi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe.


. Kuacha kushiriki ngono kwa muda. Acha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.

. Kumtibu Mwezi wako. Kuzuia maambukizi, yafaa mwezi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe.


. Kuacha kushiriki ngono kwa muda. Acha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.


ATHARI ZA PID


⚫ Ugumba kwa wanawake


⚫ Kupata Kansa ya shingo ya Uzazi.


⚫ Kutunga mimba nje ya kizazi kutokana na yai kushindwa kufika katika mji wa mimba kutokana na madhara ya PID katika mirija ya Uzazi.


⚫ KUSABABISHA majeraha nje na ndani ya mirija ya uzazi na hii hupelekea kuziba kwa mirija ya Uzazi.


⚫ Maumivu ya tumbo /ngonga mara kwa mara baada ya tendo la ndoa na kipindi cha uchavushwaji mayai (Ovulation).


JINSI YA KUEPUKA/KUJIKINGA NA PID


⚫ Epuka kuvaliana nguo za ndani.


⚫ Kuwa na tabia ya kupima mara kwa mara mfumo wako wa Uzazi.


⚫ Kuwa msafi wa mwili na nguo zako za ndan 


⚫ Kula lishe bora.


⚫ Epuka kufanya tendo la ndoa na mwenza wako mara baada ya kugundua ana magonjwa ya kujamiiana (STDs)



Tumia dawa Asili iitwayo UROGETIX 5 kwa matibabu ya haraka na uhakika ya PID.



TIBA NA USHAURI WASILIANA NASI

0755162724


Dr.Liwaya


Tiba Asili

Tanzania

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...