Skip to main content

BAWASIRI,AINA ZAKE,DALILI ZAKE,AINA ZAKE,CHANZO CHAKE NA TIBA ASILI (KUOTA KINYAMA,MIWASHO ,DAMU SEHEMU YA HAJA KUBWA)

 BAWASIRI,AINA ZAKE,DALILI ZAKE,AINA ZAKE,CHANZO CHAKE NA TIBA ASILI (KUOTA KINYAMA,MIWASHO ,DAMU SEHEMU YA HAJA KUBWA)





                            Dr.Liwaya

                         +255755162724

                  liwayaherbal@gmail.com


BAWASIRI NI NINI?

-Bawasiri ni Ugonjwa unaotokana na kuvimba/kupasuka kwa mishipa ya dawa sehemu ya haja kubwa na kupelekea kuota kwa kinyama/Uvimbe ambao ndio huitwa Bawasiri.


Sababu kubwa ya mtu kupata Bawasiri ni Mgandamizo sehemu ya haja kubwa ambapo mgandamizo huo hupelekea kupasuka/kuvimba kwa mishipa midogo midogo ya damu aina ya veins sehemu ya haja kubwa hivyo hupelekea kuota kwa kinyama,miwasho,maumivu makali na kutoa damu


 Ugonjwa huu umekuwa ni ugonjwa hatari kutokana na tabia za wagonjwa kuficha kutokana na aibu ya tatizo lenyewe lilipo au kuhofia jamii kumtazama tofauti kwa sababu jamii nyingi hasa za afrika mashariki zinaamini kuwa ugonjwa huu ni mkosi mkubwa.


   DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI

1.📎kupata muwasho mkali katika eneo la juu la haja kubwa

2.📎kujitokeza kwa kinyama/vinyama eneo la haja kubwa

3.📎kutokewa na kiuvimbe katika tundu ya haja kubwa

4.📎kupata kinyesi chenye damu

5.📎kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia

6.📎 Kupata maumivu ya tumbo/kiuno hasa Bawasiri inapofikia hatua mbaya


AINA ZA BAWASIRI⤵️

-Kuna aina 2 za Bawasiri kama ifuatavyo⤵⤵⤵⤵:

1⃣. BAWASIRI YA NJE

Ni kuota kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa ambapo kinyama huwa nje hata kama hujaenda kujisaidia haja kubwa.

2️⃣.BAWASIRI YA NDANI

Ni kuota kinyama sehemu ya ndani ya haja kubwa mara nyingi huambatana na maumivu makali na damu na kinyama hutoka wakati wa kujisaidia haja kubwa.


Bawasiri ya ndan ina hatua NNE ambazo ni:⤵⤵⤵⤵:

1. HATUA YA KWANZA

Katika hatua hii mtu hujihisi maumivu makali,miwasho pamoja na kutokwa damu wakati wa kujisaidia na kinyama hakionekan wakati wa kujisaidia.

2. HATUA YA PILI 

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe punde baada ya kujisaidia

3.HATUA YA TATU 

Hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe ama inaweza kurud yenyewe baada ya muda 

4. HATUA YA NNE

Hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi baada ya kujisaidia.


VISABABISHI/MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI

1.đź–‡️ Uzito kupita kiasi(Overweight)

2.đź–‡️ Ujauzito

3.đź–‡️ Unywaji pombe

4.đź–‡️ Kukaa sana sehemu ngumu

5.đź–‡️ Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa.

6.đź–‡️Kujisaidia Choo Kigumu.Sababu za kujisaidia choo Kigumu ni:

-Vidonda vya TUMBO

-Ngiri/Hernia

-Ulaji duni

-Kuwa na acid mwingi tumboni

7.đź–‡️ Kula sana nyama nyekundu

8.đź–‡️ Presha ya kupanda

9.đź–‡️ Kula sana pilipili

10.đź–‡️ Kula udongo(Wajawazito na watoto wadogo)

11.đź–‡️ Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa

12.đź–‡️ Kuharisha kupita kiasi.

13.đź–‡️ Kufanyakaz ngumu/kunyanyua vitu vizito


MADHARA/ATHARI ZA BAWASIRI

1.📎Upungufu wa damu mwilini

2.📎Kutokwa na kinyesi bila kujitambua 

3.📎kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa

4.📎kupungukiwa nguvu za kiume

5.📎kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu

6.📎Kupata tatizo la kisaikolojia 

7.📎Kutopata ujauzito

8.📎 Mimba kuharibika

10.📎 Kupata kansa ya utumbo ( Colorectal cancer)

11.📎 Mwili kudhoofika


NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI

1.📎Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi 

2.📎kunywa maji mengi lita 2.5 hadi 3 kwa siku

3.📎Acha kufanya mapenzi kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)

4.📎Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.

5.📎 Acha kunywa pombe

6.📎Punguza kula nyama nyekundu

7.📎Punguza matumizi ya pili pili.

8.📎Jitibie vidonda vya tumbo

9.📎 Jitibie Ngiri

10.📎 Dhibiti uzito wako

11.📎 Jiepushe/punguza kunyanyua vitu vizito mara kwa mara


MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI

Kuna matibabu aina mbili katika kutibu ugonjwa wa Bawasiri:

1.📎 MATIBABU YA KISASA

-Matibabu ya kisasa yanahusisha matibabu ya Hospital ambapo tiba kubwa ya Bawasiri kwa hospital ni kufanyiwa upasuaji mdogo ( minor surgery) kwaajili ya kuondoa kinyama. Changamoto kubwa ya matibabu haya ni kwamba asilimia kubwa ya wagonjwa wanaofanya upasuaj wa tatzo hili tatizo hujirudia kwasababu upasuaji huondoa athari ya tatzo na si mzizi wa tatizo yaani ni sawa na kukata mti kisha ukaacha mizizi bila shaka mti huo utachipua na kumea tena.Lakini pia Upasuaji wa Bawasiri huwa na maumivu makali sana na uponaji wa kidonda hufika mpaka miezi miwili,hali hii ya kukaa na kidonda kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata Kansa ya utumbo ( Colorectal Cancer).


2.📎 MATIBABU KWA NJIA ASILI

-Matibabu haya yanahusisha utumiaji wa dawa zinazotokana na mimea dawa.Dawa hizi Hutibu Bawasiri bila kufanya upasuaji na huweza kuleta matokeo ya haraka kwa mgonjwa endapo atatumia dawa huku akijitahid kujiepusha na visababishi vyote vinavyopelekea mtu kupata Bawasiri. Zipo dawa asili nyingi na nzur sana katika kutibu Bawasiri, mfano wa dawa hizo ni Bawasiri Fluid na Bawasiri powder,dawa hizi zina ufanisi mkubwa katika kutibu Bawasiri endapo Mgonjwa atazingatia maelekezo.


ZIJUE SABABU ZINAZOWAFANYA WAGONJWA WENGI WA BAWASIRI KUTUMIA DAWA NYINGI BILA MAFANIKIO

Kwanza Mgonjwa wa Bawasiri anatakiwa kufahamu ya kwamba,matibabu si dawa pekee.Watu wengi wanaamin kwamba matibabu ni dawa pekee na jambo hili limepelekea wengi kuteseka na matatzo kwa muda mrefu sana bila mafanikio na kupelekea kukata tamaa ya kutafuta tiba na badala yake humuona kila mtoa huduma ni tapeli:

Zifuatazo ni sababu zinazowafanya wagonjwa wengi kuteseka na Bawasiri kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa mbali mbali:


1.📎 Kutopata dawa sahihi 

-Si kila dawa inayotangazwa kutibu Bawasiri inaweza kutibu Bawasiri bali dawa yenye ufanisi wa kutibu ndio inaweza kutibu Bawasiri.


2.📎 Kutofuata ushaur wa daktari.

-Usipofuata yale ambayo daktari anakuelekeza ili kupata suluhisho la Tatzo lako ni ngumu kupona tatzo lako.


3.📎 Kutoziacha sababu zilizopelekea upate Bawasiri. Katika hili wengi wamefeli kwani haiwezekani ukapona Bawasiri ikiwa sababu zilizopelekea upate Bawasiri hutaki kuziacha mfano;

-Pombe

-Uzito mkubwa

-Ulaji mbovu

-Kuingiliwa kinyume 

-Kula sana pilipili

-Kukaa sana sehemu ngumu.

-Kunyanyua vitu vizito

-Kutotibu Magonjwa kama Ngiri na Vidonda vya TUMBO

-Kutokula vyakula vya kulainisha choo kama vile Mboga za majani & matunda

-Kula udongo(wajawazito)

-Kujisaidia kwenye vyoo vya kukaa.

-Kuharisha mara kwa mara

-Kujisaidia choo Kigumu


Hata utumie dawa zaid ya 100,usipoziacha sababu hizo ni ngumu sana kupona Bawasiri na matokea yake kila mtoa tiba utamuona Tapeli kumbe sababu ni wewe mwenyewe kutofuata miongozo,maelekezo na USHAURI kutoka kwa daktar.


⚫ Ukizingatia hayo utapona Bawasiri kwa muda mfupi sana(week 1 mpaka 3) Biidhnillaah japo wapo wanaopona kwa siku 5 licha ya kukaa na Bawasiri kwa miaka kadhaa .


                             Dr.Liwaya

                         +255755162724

                  liwayaherbal@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

DAWA YA KUTIBU JINO UKIWA NYUMBANI

DAWA YA KUTIBU MENO KWA HARAKA NA UHAKIKA Dawa hii imeniponesha mm mwenyewe nilikuwa nasumbuliwa na jino la juu na ndipo nilipoamua kuandaa dawa hii na imenitibu kwa HARAKA na ufanisi wa Hall ya juu sana na bado sijapatapo kuona dawa nzuri kama hii,huna haja ya kung'oa meno yako baada ya kuifahamu dawa hii eti kwasababu yanauma Mahitaji 1.✍ Mafuta ya karafuu/clove oil. 2.✍ mafuta ya Nazi/coconut oil. 3.✍ Kitunguu maji. 4.✍ Kitunguu swaum. 5.✍ Pilipili manga. 6.Chumvi ya mawe/unga wake MAANDALIZI Ponda ponda Kitunguu maji,Kitunguu swaumu,chumvi ya mawe na pilipili manga kisha changanya na mafuta na Nazi na mafuta ya karafuu kwa kiasi kidogo (robo kijiko kidogo cha chai) kisha chukua mchanganyiko huu kisha uweke juani kwa muda wa dakika 15 kisha toa juani MATUMIZI 1.ikiwa jino lina tundu chukua uji uji wa mchanganyiko huu kisha weka katika tundu na mafuta yake yapakaae pembezoni mwa jino linalouma. 2.ikiwa jina halina tundu pakaa mafuta ya mchanganyiko huu pembezoni kulizunguka jino...

TATIZO LA KUFUNGA CHOO NA KUPATA CHOO KIGUMU

Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili. Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3. Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu. Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka. Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku. Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku. Inatakiwa ifahamike kuwa ...

NI KWA NAMNA GANI BACTERIA (H.pyori) Husababisha vidonda vya TUMBO

-Bacteria, Helicobacter pylori/Campilobacter pylori_* anaweza kusafiri kutoka kwa mtu Mmoja kwenda kwa mwingine kupitia njia zifuatazo: ⤵⤵⤵ (a).📎Kupitia mate (kunyonyana midomo) (b).📎Kupitia matapishi. (c).📎 Kupitia kinyesi (d).📎Kupitia chakula ama maji yaliyokuwa na bacteria hawa. SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MTU KUAMBUKIZWA BACTERIA HAWA_ (H.pylori) ⚫ Kuishi mazingira yenye mikusanyiko mkubwa wa watu bila kuchukua tahadhar. ⚫ Kunywa maji yasiyokuwa safi. ⚫ Kula vyakula visivyooshwa mfano matunda na Mboga za majani. ⚫ Kuishi karibu na mtu mwenye vidonda vya tumbo bila kuchukua tahadhar. H.pylori anapoingia katika mwili wa binadamu huathiri uzio mwenye kulinda ukuta wa tumbo na utumbo mdogo (protective mucous) hali hii hupelekea kudhoofika kwa kuta katika tumbo na utumbo mdogo. Ukuta huu unapodhoofika husababisha Tindikali (Asidi) inayozalishwa tumbo kuunguza na kuuchimba ukuta wa tumbo pia Bacteria hawa huchimba ukuta wa tumbo na KUSABABISHA kutokea vidonda katika ukuta wa tumbo...