Skip to main content

MADHARA YA UVUTAJI WA SHISHA

Watumiaji wa kilevi cha shisha (sheesha) wako katika hatari kubwa ya kuugua maradhi ikiwemo saratani na kuathirika katika mfumo wa hewa.




Wataalamu wa afya wameonya kwamba ulevi huo ambao kwa sasa umeshika kasi na kuteka watu wengi hasa vijana, una hatari kubwa kuliko uvutaji wa sigara.

Iinasadikiwa watu wengi, hususani vijana, hivi sasa wameibukia katika uvutaji huo, wakiamini ndiyo
mbadala wa sigara kwa kudhani kuwa haina madhara.

Daktari wa Kitengo cha Matibabu ya Saratani, Hospitali ya Aga Khan, Dk Amiyn Alidina, alisema hayo kwenye majadiliano ya ufahamu wa magonjwa ya saratani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Dk Alidina alisema kilevi hicho hakina tofauti na sigara, ambayo mvutaji wake hawezi kukwepa magonjwa ya saratani, maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa hewa.

“Shisha haiwezi kuwa mbadala wa sigara kwa kudhani kuwa mtu hawezi kupata saratani na magonjwa mengine, hii ni hatari zaidi,” alisema.

Ulevi huo hutengezwa kwa kutumia chombo maalumu chenye bomba la kutolea moshi, ambacho huwekewa tumbaku, maji na moto huku ikiaminika mvuke husaidia kuchuja nguvu ya tumbaku inayoathiri mwili.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), mkupuo mmoja wa shisha una kemikali hai 4,800 na kwamba kemikali hizo husababisha saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na matatizo katika mfumo wa hewa.
Taarifa hizo za WHO zinaeleza kwamba, kiasi cha uvutaji wa shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara kati ya 100 na 200.

Hii ni kutokana na kwamba, mvutaji wa sigara hupata mikupuo kati ya minane na 12 ambayo huingiza lita 0.5 hadi 0.6 za moshi. Lakini kwa upande wa shisha, taarifa hizo za wataalamu zinaonesha anaweza kuvuta mara 200, kiasi ambacho huingiza kati ya lita 0.15 hadi moja ya moshi.

Dk Alidina anafafanua kwamba saratani imekuwa tatizo kubwa ambalo kwa kiasi kingine huchangiwa na mtindo wa maisha ambao umefanya watu kushindwa kufahamu utaratibu wa kujikinga.
Wakati huo huo alisisitiza kwamba iwapo kwenye familia ipo historia ya watu wenye saratani, inatakiwa kuwa waangalifu zaidi.

Miongoni mwa mambo ambayo jamii na familia kwa ujumla zinasisitizwa kuzingatia, ni ulaji wa matunda na kuacha matumizi ya pombe na sigara. Mtaalamu huyo pia anahimiza kufanya mazoezi ili kujiepusha na hatari ya kuugua saratani.

Wakati hapa nchini, hususani jijini Dar es Salaam, lipo wimbi kubwa la vijana wakiwemo wasichana wanaojihusisha na uvutaji wa kilevi hiki katika baa mbalimbali, vile vile taarifa kutoka maeneo mbalimbali duniani, zinaonesha kundi hili kutekwa na matumizi ya shisha.

“Uvutaji wa shisha unazidi kukua kwa sababu watu wengi hawajui madhara yake kama wanavyofahamu uvutaji wa sigara,” Profesa wa Chuo Kikuu cha London, Robert West, alikaririwa hivi karibuni na gazeti la Daily Mail la Uingereza.

MADHARA YA SHISHA

1.Kansa
Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu.

2.Matatizo ya Moyo
Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba, Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake.

3.Huharibu Fizi (periodontal disease)
Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya meno.

4. Fangasi na Kifua kikuu (TB)
Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha (hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria.

5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo)
Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji.

6. “Nicotine Addiction”
Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila kutumia shisha au sigara.

7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana.
Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa nguvu za kiume.

8.Kuchakaa kwa ngozi.
Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia.

9.Asthma na Allergy Zingine
Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma.

10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!

Wasiliana nami kwa msaada wa kiafya

+255755162724

Dr Liwaya
Dar es salaam, Ilala Pangani street.

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...