ZIJUE TOFAUTI KATI YA VIVIMBE KWENYE MFUKO WA UZAZI(FIBROIDS) NA VIVIMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI(OVARIAN CYSTS).
Vivimbe vyote katika ya fibroid na ovarian cysts huwa ni kawaida kwa wanawake, hasa kabla ya kukoma hedhi. Vivimbe kwenye mfuko wa uzazi huwa ni aina uvimbe mgumu ambao hujengeka kwenye msuli wa ukuta wa tumbo la uzazi(uterus). Kinyume chake, vivimbe maji kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts) huwa ni vifuko vyenye majimaji ambavyo huendelea kukua ndani au juu ya vifuko vya mayai. NUKUU: Na licha ya kutokea sehemu mbalimbali, dalili pekee zinaweza kukuacha ukashangaa kitu gani kibaya. Hebu tuangalie mifano yake na tofauti kati ya vivimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroids) na vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts). Tutaelezea pia kwanini ni muhimu sana kufanya vipimo. JE, DALILI ZA UVIMBE WA FIBROID NA VIUMBE KWENYE VIFUKO VYA MAYAI ZINAKUWA JE? Vivimbe vya fibroid na ovaria cysts mara nyingi huwa havisababishi dalili. Unaweza usitambue kama una vivimbe hivyo mpaka pale daktari akivigundua wakati atakapofanya vipimo. Kwa upande mwingine, kama una vivimbe vingi, au kama ...