Skip to main content

UGONJWA WA KIHARUSI, CHANZO, DALILI NA TIBA YAKE ASILIA.

Pengine umekuwa ukisikia sehemu mbalimbali kuhusu tatizo la kiharusi lakini bado hukuwahi kusoma na kuelewa vizuri. Karibu katika mfululizo wa makala zetu ambapo utajifunza nini maana ya kiharusi, aina za kiharusi, nini chanzo ama visababishi vyake. jinsi gani upunguze hatari ya kupata ugonjwa huu na huduma ya dawa za virutubisho ambavyo vitakusaidia kuondoa athari za tatizo.




Maelezo Ya Utangulizi Kwa Tatizo La Stroke
Kiharusi au stroke hutokea bila kutoa kiashiria chochote. Na ndio maana kuchukua tahadhari za kuepuka kutokea kwa tatizo ni muhimu zaidi. Kwasababu endapo utapata kiharusi na kwa bahati njema mwili ukaendela kufanya kazi basi matokeo na madhara yake yatakusumbua sana maisha yote.

Kuepuka madhara makubwa ya kiharusi mgonjwa anahitajika kutibiwa ndani ya saa moja baada ya kupata shambulizi. Hakikisha pia unafika haraka hospitali kama ukigundua moja ya dalili zifuatazo zimekutokea bila kutaraji.

Kushindwa ghafla kutembea na kupoteza balansi ya mwili.
Kuchanganyikiwa ghafla na kushindwa kufanya utambuzi
Kukosa nguvu ghafla kwa upande mmoja wa mwili
Kushindwa kuona vizuri kwa haraka
Kupata maumivu makali sana ya kichwa kwa haraka.

Kiharusi Au Stroke Ni Nini?
Kiharusi ni hali inayotokea pale mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo inapopatwa na misukosuko kiasi cha kushindwa kupeleka damu kwenye ubongo. Hali inayoathiri ufanyaji kazi wa ubongo kwa zaidi ya masaa 24.

Kulingana na shirika la afya duniani kiharusi ni nakisi katika neva ambayo hutokana na tatizo katika mishipa ya damu ya ubongo. Tatizo ambalo huendelea zaidi ya masaa 24 au kukoma ndani ya masaa 24.

Muda wa masaa 24 umechukuliwa ili kutofautisha kiharusi na kiharusi cha kukosa oksijeni katika ubongo (ischemia) ambacho hutokea na kudumu kwa muda mfupi yaani transient ischemic attack(TIA). Kwa kawaida dalili za TIA )hupotea na mtu kurudia hali yake ya kawaida ndani ya masaa 24.


Aina Za Kiharusi
Kiharusi kimegawanyika katika aina kuu mbili kulingana na jinsi kinavyotokea

Mgawanyo Wa Kiharusi Kutokana Na (Visababishi Vyake).


1.Kiharusi cha kukosa hewa kwenye Ubongo (Ischemic stroke)
Aina hii ya kiharusi hutokea iwapo usambazaji wa damu katika sehemu ya ubongo hupungua na kupelekea tishu za ubongo za eneo liliathirika kushindwa kufanya kazi zake vizuri.




Aina hii ya kiharusi husababishwa na nini? Aina hii ya kiharusi husababishwa na damu iliyoganda kuziba mishipa midogo ndani ya ubongo (cerebral thrombosis). Au kipande cha damu kumeguka na kwenda kuziba mshipa wa damu kwenye ubongo(cerebral embolism) na kupungua kwa usambazaji wa damu kwa ujumla kwa mfano shock/vena thrombosis.




2. Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya Ubongo (Hemorrhagic Stroke)

-Aina hii ya kiharusi hutokea pale ambapo mishipa midogo ya damu ndani ya ubongo hupasuka na kusababisha kusambaa kwa damu kwenye ubongo (cerebral hemorrhage). Mara nyingi aina hii ya kiharusi hutanguliwa na dalili za kichwa kuuma, au kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa.


VISABABISHI VYA KIHARUSI KWA UJUMLA

Wakati fulani, mishipa ya damu huzungukwa na aina fulani za mafuta yasiyofaa mwili, hali inayoitwa kitaalamu kama atherosclerotic plaque. Hali hii husababisha kuganda kwa damu katika mishipa (thrombosis).

Kuganda huku kwa damu kunaweza kutokea kwenye mishipa mikubwa au midogo inayopeleka damu kwenye ubongo. Baadhi ya mishipa mikubwa ya damu inayoweza kuathirika na tatizo hili ni pamoja na ateri za common carotid na interior carotid arteries, na ateri za vertebral.

Nyingine ni mishipa midogo inayounda eneo linaloitwa circle of willis lililo katika ubongo. Kuganda kwa chembe nyekundu za damu za mgojwa wa sickle cell kunaweza pia kusababisha kuziba mishipa ya damu hivyo kusababisha kiharusi.

Kuganda kwa damu
Kuganda kwa damu (embolus) kwenye mishipa ya damu ya sehemu nyingine za mwili au (hewa, mafuta, kusanyiko la vijimelea kama bakteria waletao ugonjwa wa endocarditis) huweza kusababisha kuziba kwa mishipa inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo kusababisha kiharusi.

Kupungua kwa mzunguko wa damu
-Upungufu wa usafirishaji damu mwilini (systemic hypoperfusion) .Wakati fulani moyo hushindwa kusukuma damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo ubongo kutokana na kufa kwa sehemu za nyama ya moyo kwa kukosa damu ya kutosha (Ischaemic Heart Diseases).

Au kutokana na kujaa kwa maji kwenye gamba lake la nje (pericardial effusion) au kupungua kwa damu mwilini, kunakoweza kusababishwa na mambo kadhaa. Hali hii husababisha sehemu kubwa ya mwili ikiwemo ubongo kukosa oksijeni ya kutosha na kusababisha kuathiriwa kwa sehemu ya ubongo.

Shinikizo la damu la muda mrefu lisilothibitiwa linaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa midogo inayosambaza damu kwenye ubongo na hivyo damu kujaa kwenye ubongo (Intracerebral hemorrhage).


DALILI ZA KIHARUSI

Dalili za kiharusi hutegemea na eneo la ubongo liliathiriwa. Iwapo sehemu ya ubongo mkubwa ( Cerebellum) itaathirika, mgonjwa atakuwa na dalili kama

⚫Kushindwa kutembea vizuri, hivyo kuathiri mwendo wake,
⚫Kujihisi kizunguzungu na pia kutapika.
⚫Mgonjwa atakuwa na dalili za kushindwa kuongea,kushindwa kuelewa lugha inayozungumzwa, iwapo sehemu ya ubongo wa kati (cerebral cortex) itakuwa imeathirika,
⚫Kushindwa kuona vizuri,
⚫Kuwa na ukosefu wa kumbukumbu,
⚫kuwa na mvurugiko wa mpangilio wako wa kufikiri, kuchanganyikiwa, na kubadilika kwa mwendo wa harakati za hiari.
⚫Mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na kuona; kulegea kwa misuli ya macho (aptosis)
⚫kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso; Ulegevu wa Ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande upande); kupungua uwezo wa kumeza; ulegevu wa misuli ya shingo na kushindwa kugeuza shingo upande mmoja;
⚫kushindwa kusimama sawasawa na kuona vitu kwa hali ya utofauti, , mabadiliko ya upumuaji na kiwango cha moyo kudunda, Iwapo mgonjwa ataathirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brain stem).
⚫Iwapo sehemu mojawapo ya mfumo mkuu wa neva (central nervous system) imeathirika, mgonjwa atakuwa na dalili za kupoteza ufahamu kwa upande mmoja wa mwili na kulegea kwa misuli ya uso, kuhisi ganzi mwilini, na kupungua kwa ufahamu wa hisia na hisia mtetemo. Aidha bila kujalisha eneo lililoathiriwa, mgonjwa pia anaweza kuwa na dalili za kupoteza fahamu, maumivu makali ya kichwa na kutapika. Dalili hizi za kuumwa kichwa na kutapika kwa kawaida hutokea kwa mgonjwa mwenye kiharusi cha kuvuja damu (hemorrhagic stroke) ambacho husababisha ongezeko la shinikizo na mgandamizo wa ubongo ndani ya fuvu kutokana na kuvuja kwa damu.

VIPIMO VYA KUGUNDUA TATIZO LA KIHARUSI

Vipimo Mionzi CT-scan na MRI. Vipimo vingine ni; ECG ambacho huwezesha kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia). Na kama kuna damu iliyoganda kwenye moyo ambayo inaweza kufika kwenye ubongo.

Holter monitor husaidia kutambua hitilafu katika mapigo ya moyo (arrhythmia) zinazotokea kwa vipindi. Angiogram huwezesha kugundua matatizo kwenye mishipa ya damu, na ni mishipa ipi ya damu iliyoziba. Vipimo vya damu huwezesha kutambua uwepo wa lijamu mwilini (hypercholesterolemia) na mabadiliko mengine katika damu

TABIA HATARISHI

KUTOFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Mazoezi siku hizi yamekuwa yakitumiwa na watu pekee wanao hitaji kupunguza mwili na kupunguza nyama uzembe ( belly fats) Mazoezi huimarisha viungo na mzunguko wa damu na kusaidia mwili wako kutoa taka ambazo zimepatikana kutokana na shughuli za mwili.

Tafiti zinaonesha kwamba watu ambao hawafanyi mazoezi ya kutosha katika umri mkubwa huwa hatarini kupata kiharusi aina ya ischemic. Inayosababishwa na damu kutosukumwa ipasavyo katika mishipa ya damu na kusababisha emboli kunasa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo.

ULAJI WA VYAKULA VYA WANGA NA SUKARI KUPINDUKIA

Tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa vyakula vya wanga na sukari kwa wingi husababisha uchovyaji mkubwa wa insulini. Na hivo kupelekea kiwango kikubwa cha mafuta kuhifadhiwa sehemu mbalimbali za mwili ambayo inaenda kutuathiri sana.

Lakini pia tafiti zinaonesha kwamba ulaji wa vyakula vya mafuta kama parachichi, nyama, samaki, nazi, mafuta ya olive, mafuta ya mawese, karanga na jamii zake , mboga za majani, matunda vinasaidia sana kuepukana na lehemu mbaya na kumaliza kabisa matatizo yanayo sababishwa na lehemu mbaya.

Lehemu au cholesterol kwa tafsiri nyepesi ni fati(mafuta) ambayo ipo kama nta ( wax) huzunguka sehmu mbalimbali katika mwili wako kwa kupitia mfumo wa mzunguko wa damu. Lehemu inaweza kusababisha kiharusi kwa sababu ya tabia yake ya kunasa kiurahisi kwenye kuta za mishipa ya ateri na hatimaye kupunguza kipenyo cha mshipa wa damu au kuziba kabisa na hatimaye kuzuia damu kufika vizuri katika ubongo na hatimaye ubongo hukosa damu na oxygen.

UVUTAJI WA SIGARA NA MATUMIZI YA POMBE KUPITA KIASI.

HUDUMA NA MATUNZO KWA MGONJWA WA KIHARUSI

Mojawapo ya mambo muhimu ya kufanya kwa mgonjwa aliyepata kiharusi ni kumuongoza na kumuelimisha ili arudishe ujuzi wake wa maisha ya kila siku. Hapa uhitaji ushirikiano wa wauguzi, wataalamu wa viungo, wataalamu wa ushauri wa kazi na daktari. Kuna umuhimu pia wa kuwaelimisha ndugu kuhusu hali ya mgonjwa ili waweze kumsaidia katika matunzo yake nyumbani na kwenye jamii inayomzunguka.

MATARAJIO YA TIBA ZA UGONJWA WA KIHARUSI.

Asilimia 75 ya wagonjwa wa kiharusi wanaonusurika kifo huwa walemavu na kusababisha kuathirika kwa ufanyaji kazi wao. Ulemavu unaweza kuwa wa kimwili au kiakili au vyote kwa pamoja. Ulemavu wa kimwili ni pamoja na ulegevu wa misuli, kujihisi ganzi sehemu mbalimbali za mwili hususani zilizoathirika, kujikojolea, kutoona vizuri kushindwa kuendelea na shughuli za kila siku. Ulemavu wa akili hujumuisha vitu kama mgonjwa kuwa na wasiwasi nofu ya mashambulizi, na Uunyonge.


MATIBABU YA KIHARUSI

1. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na ubongo kukosa hewa (Ischemic stroke) Mgonjwa hutibiwa kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu iliyoganda (thrombolytics) au kwa kuondoa damu iliyoganda kwa njia mbalimbali (thrombectomy). Dawa nyingine kama vile junior Aspirin na Clopidogrel hutolewa kwa ajili ya kuzuia chembe sahani kukusanyika na kuganda.

2. Matibabu ya kiharusi kinachotokana na damu kuvujia kwenye ubongo (Hemorrhagic stroke) Aina hii ya kiharusi huitaji tathmini ya upasuaji wa neva ili kuchunguza na kutibu sababu ya damu kuvuja. Angalizo: kumpa mgonjwa wa aina hii ya kiharusi dawa za kuyeyusha damu iliyoganda au za kuzuia kuganda maana inhatarisha maisha ya mgonjwa badala ya kumsaidia. Kwahiyo ni vizuri kwa wataalamu kufanya ufanya uchunguzi wa kutosha ili kuwa na uhakika na tatizo.

MATIBABU YA KIHARUSI KWA KUTUMIA DAWA ZA MIMEA

Tafiti zinasema kwamba dawa za mimea zinaleta matokeo mazuri zaidi katika kutibu tatizo la kiharusi na mgonjwa kupata nafuu kwa karibu asilimia 70%. Wasiliana nasi tuweze kukupatia na muongozo mzuri wa kumaliza kabisa tatizo la kiharusi

+255755162724
Dr Liwaya

Dar es salaam, Ilala Pangani street


Comments

Popular posts from this blog

NI KWA NAMNA GANI BACTERIA (H.pyori) Husababisha vidonda vya TUMBO

-Bacteria, Helicobacter pylori/Campilobacter pylori_* anaweza kusafiri kutoka kwa mtu Mmoja kwenda kwa mwingine kupitia njia zifuatazo: ⤵⤵⤵ (a).📎Kupitia mate (kunyonyana midomo) (b).📎Kupitia matapishi. (c).📎 Kupitia kinyesi (d).📎Kupitia chakula ama maji yaliyokuwa na bacteria hawa. SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MTU KUAMBUKIZWA BACTERIA HAWA_ (H.pylori) ⚫ Kuishi mazingira yenye mikusanyiko mkubwa wa watu bila kuchukua tahadhar. ⚫ Kunywa maji yasiyokuwa safi. ⚫ Kula vyakula visivyooshwa mfano matunda na Mboga za majani. ⚫ Kuishi karibu na mtu mwenye vidonda vya tumbo bila kuchukua tahadhar. H.pylori anapoingia katika mwili wa binadamu huathiri uzio mwenye kulinda ukuta wa tumbo na utumbo mdogo (protective mucous) hali hii hupelekea kudhoofika kwa kuta katika tumbo na utumbo mdogo. Ukuta huu unapodhoofika husababisha Tindikali (Asidi) inayozalishwa tumbo kuunguza na kuuchimba ukuta wa tumbo pia Bacteria hawa huchimba ukuta wa tumbo na KUSABABISHA kutokea vidonda katika ukuta wa tumbo...

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME, CHANZO, DALILI NA TIBA YAKE ASILIA

Ufafanuzi wa jumla wa tatizo la nguvu za kiume na tiba yake​ Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa, au kuwahi kufika kileleni. Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka siku had I siku. Tafiti mbalimbali zinasema wanaume wengi wenye umri kuanzia miaka 35 na kuendelea ndio wanaosumbuliwa na tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kutokana na kwamba wengi wao wanakuwa hawaelewi aina ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla, namna wanavyotakiwa kuishi ili kupunguza janga hilo, wanakunywa pombe na hawajishughulishi na mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo hupunguza tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kwa asilimia kubwa sana. Kupungukiwa nguvu za kiume kunaweza pia kuwa kumetokana na mambo ya kihisia, kwa kiingereza ‘emotional causes’. Vitu vingine vinavyoweza kusababi...

DAWA YA KUTIBU JINO UKIWA NYUMBANI

DAWA YA KUTIBU MENO KWA HARAKA NA UHAKIKA Dawa hii imeniponesha mm mwenyewe nilikuwa nasumbuliwa na jino la juu na ndipo nilipoamua kuandaa dawa hii na imenitibu kwa HARAKA na ufanisi wa Hall ya juu sana na bado sijapatapo kuona dawa nzuri kama hii,huna haja ya kung'oa meno yako baada ya kuifahamu dawa hii eti kwasababu yanauma Mahitaji 1.✍ Mafuta ya karafuu/clove oil. 2.✍ mafuta ya Nazi/coconut oil. 3.✍ Kitunguu maji. 4.✍ Kitunguu swaum. 5.✍ Pilipili manga. 6.Chumvi ya mawe/unga wake MAANDALIZI Ponda ponda Kitunguu maji,Kitunguu swaumu,chumvi ya mawe na pilipili manga kisha changanya na mafuta na Nazi na mafuta ya karafuu kwa kiasi kidogo (robo kijiko kidogo cha chai) kisha chukua mchanganyiko huu kisha uweke juani kwa muda wa dakika 15 kisha toa juani MATUMIZI 1.ikiwa jino lina tundu chukua uji uji wa mchanganyiko huu kisha weka katika tundu na mafuta yake yapakaae pembezoni mwa jino linalouma. 2.ikiwa jina halina tundu pakaa mafuta ya mchanganyiko huu pembezoni kulizunguka jino...