Ujauzito huja na tabia nyingi ambazo baadhi huwa za kawaida huku baadhi zikiwa siyo za kawaida. Ni muhimu sana kwa mama mjamzito kuzungumza na daktari mara kwa mara ili kuondoa sintofahamu hizi ambazo siyo nzuri kwa afya. Tumekuletea dalili za hatari wakati wa ujauzito ambazo ni lazima zishughulikiwe haraka ili kuzuia madhara makubwa yanayoweza kutokea kwa mama na mtoto. 1. Damu kwenye via vya uzazi Katika mazingira ya kawaida, damu huwa haipaswi kutoka wakati wote wa ujauzito. Katika mazingira fulani, siku ya 10-14 baada ya kutungwa kwa ujauzito mwanamke anaweza kutokwa na damu kidogo ambayo humaanisha kuwa kijusi kinajishikiza kwenye mji wa uzazi ili kianze kulelewa. Kutokwa na damu kwenye via vya uzazi muda wowote mwingine siyo ishara nzuri hivyo inapawa kuchukuliwa kama jambo la dharura. Baadhi ya sababu zinazoweza kufanya damu itoke ni uwepo wa maambukizi makubwa, tishio la kuharibika kwa ujauzito, kuwa na ujauzito unaolelewa nje ya mji wa uzazi au uwepo wa changamoto zozote kweny...
Tuna wasaidia wahanga wa magonjwa mbalimbali kupona magonjwa yao kwa kutumia tiba asilia pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu.