Skip to main content

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA)


Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?."

Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?"

Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?"

Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine mkongo nk.

Lakini swali linakuja je kuna madhara yoyote?

Jibu ni ndiyo kuna madhara makubwa sana kiafya.

Wanaume wengi ninaozungumza nao wanasema kinachowavuta kutumia dawa hizo ni
- Wanakosa hamu ya tendo la ndoa. Hata mwanamke akiwepo hamu inapotea
- Wanawahi sana kumaliza. Dakika moja,mbili tatu umemaliza.
- Uume unasimama vizuri ila unakuwa legelege
- Wanakosa uwezo wa kurudia bao la pili, la tatu na kuendelea
- Wanakosa nguvu za kiume kwa ujumla

Madhara yenyewe ni haya hapa👇👇

1️⃣ UNAPOTUMIA DAWA HIZO UNATENGENEZA UBONGO NA MWILI WAKO KUWA TEGEMEZI. 


Ubongo ndio huongoza mwili na kuratibu shughuli zote za mwili ikiwa ni pamoja na sex. Kwahiyo ubongo ukizoea kuongoza mwili wako ufanye sex ukiwa umetumia dawa hizo za kuboost, maana yake ni kwamba miaka yote wewe bila kutumia dawa huwezi.

Pia unakuwa na woga sana, kwamba usipotumia dawa huwezi. Unaanza kujidharau, na kukosa furaha , wengine mashahidi humu kuna wanawake wengine wakikugundua kuwa unatumia hizo dawa kabla ya kufa mapenzi wanakuonesha dharau,matusi hadi kuachana kabisa.

2️⃣ UNAPOTUMIA VIDONGE HIVYO UNAKUSANYA WINGI WA KEMIKALI MWILINI MWAKO AMBAZO KADIRI ZINAVYO RUNDIKANA HULETA MADHARA MAKUBWA KIAFYA. 

Zile dawa hutengenezwa kwa kutumia formula za kikemikali,ambazo hupelekea matatizo mengine kama vile ganzi, na kupooza upande mmoja wa mwili.

Hii husababishwa na zile kemikali au mabaki ya dawa, ambazo husafirishwa kwa damu na kwenda sehem za mikono, miguu na kichwani.

Kwahiyo kupoteza fahamu ,miguu kuuma na kufa ganzi, nk ni moja kati madhara ya kutumia dawa hizo. 

3️⃣ UNAUA KABISA UWEZO WAKO WA KUFANYA TENDO LA NDOA. KUNA WAKATI HUTOWEZA HATA KUSIMAMISHA UUME. 

Hamu ya tendo la ndoa ni mchakato mrefu, tutajifunza hapa.
Hivyo kwa kutumia dawa hizo unaharibu mwili kabisa na kupoteza uwezo wa kufanya mapenzi bila kutumia dawa, 

mwisho hupelekea kukosa nguvu kabisa hata kama utatumia dawa hutaona uume hauna nguvu wala haupati hamu ya tendo la ndoa.

4️⃣ UNAHARIBU UBORA WA MBEGU AU MANII HIVO HUPELEKEA UGUMBA.

Mbegu za kiume ili zianguliwe zikiwa bora hutegemea kile kinachoingia.

Na dawa hizi hufanya kazi kwenye mfumo mzima wa uzazi yaan korodan, mishipa yote ya uume, na tezi dume ambalo huhusika kutoa ule ute mlainii mweupe kabla ya kufanya mapenzi na wakati wa kutoa mbegu.

Sasa kama korodan zitaathirika, tezi dume, na mishipa basi mbegu pia hutoka zikiwa hazina ubora , chache, nyepesi kama maji maji, na hivyo ukipimwa utaambiwa hauna mbegu nzuri za kutungisha mimba. Unakaa ndani ya ndoa miaka mingi mtoto hakuna jiulize.

5️⃣ UNAHARIBU MISULI YA UUME WAKO, HIVYO KUNA WAKATI HATA UTUMIE DAWA MISULI HAITAWEZA KUWA NA NGUVU KABISA

Wakati unafanya mapenzi muda mrefu bila kumwaga kwa kusaidiwa na dawa unaona ni ufahari, lakini ukweli ni kwamba mishipa Ile ya uume Mungu aliiumba iweze kufanya kazi kwa muda sahihi ambao hauna madhara kwenye mishipa.

6️⃣ IKIWA MTUMIAJI ANA MAGONJWA MENGINE HUPELEKEA KIFO. HASA MAGONJWA SUGU KAMA MAGONJWA YA MOYO, PRESSURE, SUKARI.

Tendo la ndoa huhusisha mzunguko wa damu. Ikiwa utalazimisha damu izunguke kwa nguvu kuzidi uwezo wa mwili wako maanayake moyo utashindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa.

Mwisho hupelekea mwili hukosa nguvu ghafla, hali ambayo hupelekea kifo cha ghafla.

7️⃣ MATUMIZI YA DAWA HIZO HUPELEKEA MATATIZO YA MACHO NA MASIKIO.

Mzunguko wa damu hupelekea kupekea zile sumu za dawa kufika mpaka kichwani kwenye mishipa ya masikio na macho. Hivyo husababisha kuathiri ubongo na mishipa inayopeleka taarifa sehem zote za kichwa , masikio na macho.hivyo maumivu ni hali ya hatari

8️⃣ MAUMIVU YA KICHWA YA MARA KWA MARA.

Kichwa kuuma kitaalam huashiria mambo mawili, moja ni kichwa kuuma kinatoa taarifa kuwa sehem flan kwenye mwili wako kuna tatizo la kiafya , inawezekana kwenye mfumo wa mzunguko wa damu au moyo au magonjwa mengine nje na magonjwa yatokanayo ma shida za moyo kushindwa kufanya kazi vizuri.

Pili kichwa kuuma ni kwamba kuna magonjwa yanayohusu kichwa chenyewe. Kama nilivoelezea kwenye dondoo #7

Kwahyo unapotumia dawa hizo tegemea kupata hali hiyo.

Ok
Kwahiyo kitaalam haishauriwi kutumia dawa hizo bila kuhusiwa na daktari, ni mpaka utakapopimwa na kupewa maelekezo sahihi ya kutumia, ikiwa ni pamoja na muda gani wa kutumia, na namna sahihi ya kutumia,na nini hupaswi kufanya ikiwa unatumia dawa hizo,

Pia kuna baadhi ya watu ambao hawaruhusiwi kabisa kuzitumia kwa namna yoyote ile.

Kwahiyo, daktari atakwambia utumie ikiwa kuna kuna ulazima kulingana na afya yako kwa ujumla. Pamoja na makatazo mengine atakayokupa ili uwe salama.

Ndani ya group hapa tutajifunza na masomo mengine nimekwisha anza kuwafundisha hapa tangu jana na leo njia rahisi za kutibu tatizo hilo.

kwa wale watakaofuatilia hatua kwa hatua na kuchukua hatua kufanyia kazi watapona kabisa kwasababu mmeona baadhi ya shuhuda za wanaume wachache waliozingatia.

Kutatua changamoto hiyo, tengeneza dawa ninazofundisha hapa tumia ukiwa nyumbani kwako.

Pia ikiwa unahitaji dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja ipo, ninauza Ni dawa iliyotengenezwa kwa mimea tiba kwaajili ya kutatua changamoto hiyo moja kwa moja. waweza kuwasiliana nami kunifafanulia tatizo lako kwa kina zaidi

+255755162724
Dr Liwaya

Dar es salaam
Ilala boma
Pangani Street..

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...