Skip to main content

VYAKULA AMBAVYO NI VIZURI SANA KWENYE KUSAIDIA NA KUIMARISHA MFUMO WA UZAZI WA MWANAUME

 VYAKULA AMBAVYO NI VIZURI SANA KWENYE KUSAIDIA NA KUIMARISHA MFUMO WA UZAZI WA MWANAUME




NAFAKA

●Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone, pia huwezesha mtu kuwa na nguvu tele hatimaye kuongeza nguvu zake za kiume kutokana na virutubisho mwili unavyopata. 


▪︎Vyakula vya nafaka vimesheheni nishati nyingi, nafaka zina nyuzinyuzi (fibres) na sukari

ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili.


▪︎Kula nafaka zisizokobolewa kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi

badala ya cornflakes ni jambo zuri kiafya zina saidia kutokupa mwili wa mafuta mengi, 


▪︎ikumbukwe uwepo wa mafuta mabaya yana athiri mishipa ya damu ikiwamo ya uume.



TANGAWIZI

●Tangawizi ni aina ya kiungo mizizi ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. 

▪︎Mzunguko unapokuwa mzuri huwezesha damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi ikiwamo uume. 


▪︎Tangawizi imekuwa ikitumika sana maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu

za kiume. 


▪︎Pia baadhi ya Viungo ambavyo viko katika pilau ni mojawapo ya vitu ambavyo miaka na miaka imetumika

maeneo ya Asia na Amerika ya Kaskazini kama viungo vyakula vinavyoimarisha nguvu za kiume.



KOMAMANGA

●Komamanga (Pemigranate) ni aina ya matunda yenye rangi nyekundu na mwonekano kama apple. 


●Tunda hili husaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumwongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa. 


●Hivyo humfanya mtumiaji kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi.



*MBEGU MBALI MBALI ZA MATUNDA, IKIWEMO TIKITIMAJI NA MBEGU ZA MABOGA*

●Mchanganyiko wa mbegu mbalimbali za matunda ikiwamo tikiti maji na mbegu za maboga husaidia

kuondoa ACID mwilini na kuupa mwili virutubisho tele vinavyoimarisha afya ya uzazi wa mwanaume na kumfanya mtu awe mwenye afya njema.



ASALI

●Asali Ina madini yanayoitwa boron ambayo husaidia mwili kutumia homoni. 


●Hata vitabu vya dini hueleza ulaji wa asali na masega yake kama mlo wenye kuupa mwili nguvu. 


•Pia Zipo tafititi lukuki kuhusu faida za asali, faida mojawapo ikiwamo  kusaisia kuongeza nguvu za kiume.



KARANGA

●Karanga.

-Huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya. Husaidia

kuimarisha mzunguko wa damu katika maeneo ya uzazi 


▪︎hivyo kuongeza msisimko wa tendo.

▪︎Pia karanga zina madini muhimu kama vile madini ya magineziamu, tindikali ya foliki na madini ya zinki ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume na kuongeza hisia.



BLUEBERRY

●Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita "viagra asilia" kutokana na kazi inayoifanya mwilini. 


●Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini.

▪︎ Damu ndio kila kitu katika nguvu

za kiume. 


▪︎Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi ambazo husaidia kuondoa kolesteroli

(Cholestrol) mwilini kabla haijanganda kwenye mishipa ya damu. 


▪︎Kuwa na mzunguko mzuri wa

damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi.



MTINI (FIGS)

●Mtini (Figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika

kuzalisha homoni mwilini. 


●Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. 


●Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.



VITUNGUU SAUMU

●Vitunguu saumu vina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo

vya uzazi. 


●Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina katika tendo la ndoa.



NDIZI

●Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. 


●Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. 


●Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi

(libido).



MIZIZI YA MACA

●Maca Root Ni mmea maarufu sana huko Brazil ambao umekua ukitumiwa na wanaume na wanawake wengi ili kuwapa nguvu ya muda mrefu,kuondoa stress,afya ya uzazi,kubalance hormone,na kuwapa

hamu ya tendo la ndoa,n.k

N.k....

●Binafsi ninashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo yako yote ya kiafya. Mwili una njia

zake za kurekebisha kila kitu. 


▪︎Ukiona kuna tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa

kurekebishwa. 


▪︎Kutumia madawa makali hudhoosha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa

kufanya kazi kama inavyotakiwa. 


▪︎Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna

kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.



đź“ŚMara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu kuleta mabadiliko, lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hu-BOOST na hayatibu.


Dr Liwaya

0755162724

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...