Skip to main content

UVIMBE KWENYE KIZAZI,SABABU ZAKE, DALILI ZAKE NA TIBA YAKE ASILI

TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI,SABABU, DALILI NA TIBA YAKE ASILI




FIBROID NI NINI?


Siku hizi kuna ongezeko kubwa sana la huu ugonjwa hebu tega sikio.

Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.



Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.


Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.


Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.


SABABU ZA MWANAMKE KUPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI


Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;


1. 📎Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini.

2.📎 Ujauzito.

3.📎 Uzito/ unene kupita kiasi.

4.📎 Jenetiki zisizo za kawaida.

5.📎 Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu.

6.📎 Sababu za kurithi.

7.📎 Lishe isiyo sawa/Lishe duni.

8.📎Sumu na taka mbalimbali mwilini.



AINA ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI

Kuna aina kuu 3 za uvimbe kwenye kizazi kama ifuatavyo:


1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi)


2.Intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi)


3.Subserosal(nje ya kizazi)


WAFUATAO WAPO HATARINI KUPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI(UTERINE FIBROID)

1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa

2.miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma

3.kurithi

4.Unene/uzito kupita kiasi

5.kuingia hedhi mapema


Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto.

Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma.



DALILI ZA MWANAMKE MWENYE UVIMBE KWENYE KIZAZI (UTERINE FIBROIDS):


1.đź–‡️Kupata damu nyingi wakati wa hedhi.

2. đź–‡️Maumivu makali wakati wa siku za hedhi.

3. đź–‡️Kuvimba miguu.

4. Unaweza kuhisi una ujauzito.

5. đź–‡️Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

6. đź–‡️Kuhisi kuvimbiwa.

7. đź–‡️Kupata haja ndogo kwa taabu.

8. đź–‡️Kutokwa na uchafu ukeni.

9.đź–‡️ Kupata choo kigumu au kufunga choo.

10.đź–‡️ Maumivu nyuma ya mgongo.

11. đź–‡️Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto.

12.đź–‡️ Upungufu wa damu.

13.đź–‡️ Maumivu ya kichwa.

14.đź–‡️ Uzazi wa shida.

15.đź–‡️ Kutopata ujauzito.

16.đź–‡️ Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo.

17.đź–‡️ Maumivu ya nyonga.

18.đź–‡️ Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage).

19.đź–‡️ Kukojoa mara kwa mara kwan uvimbe huweka mgandamizo katika kibofu cha mkojo

20.đź–‡️ Hedhi zisizokuwa na mpangilio


MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUPONA HARAKA UVIMBE KWENYE KIZAZI


1. 📎Hakikisha una uzito sawa kila mara kulingana na urefu wako.

2. 📎Kula sana mboga za kijani na matunda

3. 📎Fanya mazoezi ya viungo kila mara, mara 4 mapaka 5 kwa wiki

4. 📎Kunywa maji mengi kila siku lita mbili mpaka lita tatu

5. 📎Kula sana vyakula vyenye nyuzi nyuzi (faiba) na punguza vyakula vyenye mafuta

6. 📎Usitumie bidhaa zozote zenye kaffeina (chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote nk), nyama nyekundu na vyakula vya kuchomwa au kupikwa katikati ya mafuta mengi (maandazi, chipsi, nk)

7. 📎Achana kabisa na mawazo mawazo (stress) na hamaki nyingine zozote

8. 📎Acha kuvuta sigara/tumbaku na vilevi vingine vyote hadi hapo utakapopona kabisa



MATIBABU/TIBA ASILI KWA UVIMBE KWENYE KIZAZI.


Tiba asili ndio njia salama na rahisi katika matibabu ya uvimbe kwenye kizazi endapo mgonjwa atafuata ushauri na matumizi sahihihi ya dawa.


Zipo dawa asili zenye ufanisi mkubwa sana katika kutibu uvimbe kwenye kizazi, Mfano ni dawa hizo ni FIBROCYST SOLUTION nk hii ni dawa yenye uwezo mkubwa sana katika kutibu uvimbe kwenye kizazi.


Wasiliana nami kwa Ushaur, matibabu na miongozo mbali mbali ya kitabibu:


Dr.Liwaya

Tiba asili

Tanzania


+255755162724

liwayaherbal@gmail.com


Tunapatikana Dar Es salaam

Comments

Popular posts from this blog

ZIJUE FAIDA,MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU

MAGONJWA YANAYOTIBIKA KUPITIA KITUNGUU SAUMU Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro) Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine Huzuia kuhara damu (Dysentery) Huondoa Gesi tumboni Hutibu msokoto wa tumbo Hutibu Typhoid Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi Hutibu mafua na malaria Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB) Hutibu kipindupindu Hutibu upele Huvunjavunja mawe katika figo Hutibu mba kichwani Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume) Hutibu maumivu ya kichwa Hutibu kizunguzungu Hutibu shinikizo la juu la damu Huzuia saratani/kansa Hutibu maumivu ya jongo/gout Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula Huongeza hamu ya kula Huzuia damu kuganda Husaidia kutibu kisukari Husaidia kutibu ...

TATIZO LA KUFUNGA CHOO NA KUPATA CHOO KIGUMU

Tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu ni jambo tunalolikwepa kwenye mazungumzo yetu ya kila siku. Hata hivyo ni tatizo kubwa katika jamii na mbaya zaidi wengi hawajuwi madhara yake ni nini ya kuendelea kulivumilia tatizo hili. Kupata choo kigumu au kufunga choo ni ishara ya tatizo lingine baya zaidi mwilini. Kama kuna jambo unapaswa uliepuke kwa nguvu zote basi ni hili. Kwa afya bora kabisa hakikisha unapata choo kila siku mara 2 hata mara 3. Choo kilaini siyo kigumu na chenye maumivu. Wakati mwingine utakapopata tatizo hili naomba usiwe na aibu kulisema wazi hata kwa boss wako ili upate matibabu kwa haraka. Kufunga choo au kupata choo kigumu ndiyo CHANZO KIKUU CHA UGONJWA WA BAWASIRI kwa waTanzania wengi na hii inachangiwa kwa sehemu kubwa kwa kula ugali wa sembe na kutokunywa maji mengi kila siku. Pamoja na hayo, hakuna ugonjwa rahisi kutibika kama huu ikiwa utaamua kushughulisha kichwa chako kidogo hasa kwa kuangalia unakula na kunywa nini kila siku. Inatakiwa ifahamike kuwa ...

UGONJWA WA KIHARUSI, CHANZO, DALILI NA TIBA YAKE ASILIA.

Pengine umekuwa ukisikia sehemu mbalimbali kuhusu tatizo la kiharusi lakini bado hukuwahi kusoma na kuelewa vizuri. Karibu katika mfululizo wa makala zetu ambapo utajifunza nini maana ya kiharusi, aina za kiharusi, nini chanzo ama visababishi vyake. jinsi gani upunguze hatari ya kupata ugonjwa huu na huduma ya dawa za virutubisho ambavyo vitakusaidia kuondoa athari za tatizo. Maelezo Ya Utangulizi Kwa Tatizo La Stroke Kiharusi au stroke hutokea bila kutoa kiashiria chochote. Na ndio maana kuchukua tahadhari za kuepuka kutokea kwa tatizo ni muhimu zaidi. Kwasababu endapo utapata kiharusi na kwa bahati njema mwili ukaendela kufanya kazi basi matokeo na madhara yake yatakusumbua sana maisha yote. Kuepuka madhara makubwa ya kiharusi mgonjwa anahitajika kutibiwa ndani ya saa moja baada ya kupata shambulizi. Hakikisha pia unafika haraka hospitali kama ukigundua moja ya dalili zifuatazo zimekutokea bila kutaraji. Kushindwa ghafla kutembea na kupoteza balansi ya mwili. Kuchanganyikiwa ghafla n...