Skip to main content

TATIZO LA KUKOMA KWA HEDHI

Nini Maana Ya Kukoma Hedhi?
 




Kukoma hedhi ni hali ya kawaida ambayo wanawake wote huipitia umri ukiwa mkubwa. Neno kukoma hedhi linaweza likaelezea mabadiliko yo yote yanayomtokea mwanamke muda mfupi kabla au baada ya kuacha kupata siku zake, ikiwa ni ishara ya mwisho wa kuzaa.



Nini Kinasababisha Kukoma hedhi?
 

Mwanamke huzaliwa akiwa na idadi kamili ya mayai, ambayo hutunzwa ndani ya ovari. Ovari hizi pia hutengeneza homoni za estrogen na progesterone, ambazo husimamia hedhi na upevushwaji wa mayai. Kukoma hedhi maana yake ovari kukoma kuachia yai kila mwezi na kusimama kuingia mwezini.

Kukoma hedhi ni sehemu ya kawaida ya mwili kuzeeka na hutokea baada ya kufikia umri wa mika 40. Lakini baadhi ya wanawake wanawake wanaweza kukoma hedhi mapema zaidi, ikiwa ni matokeo ya upasuaji, kama hysterectomy, au uharibifu kwenye ovari, kama baada ya tiba ya chemotherapy. Kukoma hedhi kabla ya miaka 40, kwa sababu yo yote ile huitwa premature menopause.



Dalili Za Kukoma Hedhi
 

Wanawake wengi wanaokaribia kukoma hedhi wanapata hot flashes, yaani ghafla kusika joto linalosambaa sehemu ya juu ya mwili, vikiambatana na hali ya kutahayari na kutokwa jasho. Hali hii huwa si kali sana kwa wanawake wengi lakini kwa wengine huwa mbaya.


Dalili nyingine zinazotokea mwanamke anapokaribia kukoma hedhi ni pamoja na:

  1. Hedhi zisizo na mpangilio au zinazorukaruka
  2. Kukosa usingizi
  3. Kusikia hasira mara kwa mara
  4. Uchovu
  5. Mfadhaiko
  6. Moyo kwenda mbio
  7. Maumivu ya kichwa
  8. Maumivu ya joints na misuli
  9. Mabadiliko katika kusikia hamu ya tendo la ndoa
  10. Uyabisi wa uke
  11. Shida kudhibiti haja ndogo

Si wanawake wote wanaopata dalili hizi zote.


KUKOMA KWA HEDHI KUNAANZA UMRI GANI? 

Wanawake wengi huanza kupata dalili za kukoma kwa hedhi kati ya umri wa miaka 45 hadi 55 lakini katika hali isiyo ya kawaida wengine wanaweza kupata hata kabla ya kutimiza umri wa miaka 40.

Shirika hilo hata hivyo linasema si rahisi kutabiri ni lini mwanamke atafikia ukomo wa hedhi ijapokuwa kuna uhusiano kati ya umri na vigezo kama vile afya na jenetiki.

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wanawake wanaofikia ukomo wa hedhi inaongezeka ambapo mwaka 2021 wanawake wenye umri wa miaka 50 na kuendelea walikuwa asilimia 26 ya wanawake na wasichana wote duniani kote.

Idadi hiyo ni sawa na ongezeko kwa asilimia 22 ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita.

Halikadhalika wanawake wanaishi muda mrefu zaidi ambapo mwanamke aliyekuwa na umri wa miaka 60 mwaka 2019 anatarajiwa kuishi kwa wastani wa miaka mingine 21.


Usikose kuuliza maswali wakati wo wote kuhusiana na mada zetu, tutafurahi sana kuona kuwa tumekujibu vyema.

 

Kwa maswali zaidi na ushauri piga 0755 162 724

Au bonyeza link ya WhatsApp ipo mwisho upande wa kulia wa makala hii.

Comments

Popular posts from this blog

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...

MADHARA YA ZA KUBOOST NGUVU ZA KIUME

JE, KUNA MADHARA YOYOTE KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU KWA MUDA ? (DAWA ZA KOBOOST NGUVU KWA MUDA) Nimekuwa nikipokea swali hili ,"mimi natumia sana dawa kuboost au kunipa nguvu ninapohitaji kwenda kufanya mapenzi. Je, kuna madhara yoyote?." Mwingine anauliza .."samahan mimi nimetumia sana dawa za kunipa hamu wakati wa tendo la ndoa lakini saizi najikuta siwezi kabisa uume hauna nguvu hata nikitumia dawa nilizozoea kutumia bado sipati nguvu, je tatizo nini?" Mwingine huyu hapa, "Kila nikihitaji kufanya sex lazima nitumie mkongo ,au vumbi la kongo. Je wewe una dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja mpaka nikawa na nguvu za kiume vizuri niachane na mkongo kabisa?" Jamani hayo hapo ni baadhi tu ya maswali mengi ninayoulizwa, na nimetambua kuwa zaidi ya wanaume 25,000 ambao nawapa elimu hii, idadi kubwa sana wamekumbwa na tatizo hili la uraibu (addiction) wa kutumia dawa za kuboost uwezo wa kufanya sex, wengine wanatumia vidonge vya kizungu kama Viagra, wengine ...

ZIFAHAMU FAIDA MUHIMU ZA ASALI

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, jarida la World News limeandika kuwa asali inauwezo mkubwa wa kutibu kama itachanganywa na mdalasini. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork ambapo mchanganyiko huo unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, amesema madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini. Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwa...