Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2023

TATIZO LA KUKOMA KWA HEDHI

Nini Maana Ya Kukoma Hedhi?   Kukoma hedhi ni hali ya kawaida ambayo wanawake wote huipitia umri ukiwa mkubwa. Neno kukoma hedhi linaweza likaelezea mabadiliko yo yote yanayomtokea mwanamke muda mfupi kabla au baada ya kuacha kupata siku zake, ikiwa ni ishara ya mwisho wa kuzaa. Nini Kinasababisha Kukoma hedhi?   Mwanamke huzaliwa akiwa na idadi kamili ya mayai, ambayo hutunzwa ndani ya ovari. Ovari hizi pia hutengeneza homoni za estrogen na progesterone, ambazo husimamia hedhi na upevushwaji wa mayai. Kukoma hedhi maana yake ovari kukoma kuachia yai kila mwezi na kusimama kuingia mwezini. Kukoma hedhi ni sehemu ya kawaida ya mwili kuzeeka na hutokea baada ya kufikia umri wa mika 40. Lakini baadhi ya wanawake wanawake wanaweza kukoma hedhi mapema zaidi, ikiwa ni matokeo ya upasuaji, kama hysterectomy, au uharibifu kwenye ovari, kama baada ya tiba ya chemotherapy. Kukoma hedhi kabla ya miaka 40, kwa sababu yo yote ile huitwa premature menopause. Dalili Za Kukoma Hedhi   Wanawake wengi w...

NI KWA NAMNA GANI BACTERIA (H.pyori) Husababisha vidonda vya TUMBO

-Bacteria, Helicobacter pylori/Campilobacter pylori_* anaweza kusafiri kutoka kwa mtu Mmoja kwenda kwa mwingine kupitia njia zifuatazo: ⤵⤵⤵ (a).đź“ŽKupitia mate (kunyonyana midomo) (b).đź“ŽKupitia matapishi. (c).đź“Ž Kupitia kinyesi (d).đź“ŽKupitia chakula ama maji yaliyokuwa na bacteria hawa. SABABU ZINAZOWEZA KUPELEKEA MTU KUAMBUKIZWA BACTERIA HAWA_ (H.pylori) ⚫ Kuishi mazingira yenye mikusanyiko mkubwa wa watu bila kuchukua tahadhar. ⚫ Kunywa maji yasiyokuwa safi. ⚫ Kula vyakula visivyooshwa mfano matunda na Mboga za majani. ⚫ Kuishi karibu na mtu mwenye vidonda vya tumbo bila kuchukua tahadhar. H.pylori anapoingia katika mwili wa binadamu huathiri uzio mwenye kulinda ukuta wa tumbo na utumbo mdogo (protective mucous) hali hii hupelekea kudhoofika kwa kuta katika tumbo na utumbo mdogo. Ukuta huu unapodhoofika husababisha Tindikali (Asidi) inayozalishwa tumbo kuunguza na kuuchimba ukuta wa tumbo pia Bacteria hawa huchimba ukuta wa tumbo na KUSABABISHA kutokea vidonda katika ukuta wa tumbo...

TATIZO LA MAWE KWENYE MFUKO WA NYONGO

JINSI YA KUDHIBITI TATIZO LA MAWE KWENYE MFUKO WA NYONGO Kabla ya kulifahamu tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo,hebu kwanza fahamu kwa ufupi nyongo ni nini na kazi yake ni ipi. Si hivyo tu bali pia nataka ufahamu mfuko wa nyongo ni nini na una kazi gani ndipo ufahamu jinsi mawe yanavyotokea kwenye mfuko wa nyongo. NYONGO( BILE) NI NINI? Nyongo ni juisi inayotumika kumeng'enyea chakula ambayo huzalishwa na ini na kutunzwa ndani ya mfuko wa nyongo. Nyongo haina kimeng'enya (enzymes) lakini ina asidi inayosaidia kumeng'enya mchanganyiko wa mafuta mwilini. KAZI ZA NYONGO Nyongo ina kazi kubwa mbili: Kusaidia umeng'enywaji wa mafuta na kusharabiwa kwenye utumbo mwembamba-Chumvi chumvi iliyo kwenye nyongo hujishikiza na mafuta yanayotokana na chakula na kupenya kuingia kwenye mishipa ya damu na badaye hurejeshwa kwenye nyongo. Kusaidia kutoa uchafu nje toka kwenye damu- Mwili una kawaida ya kuvunja chembe hai nyekundu za damu zilizozeeka na kutengeneza mpya. Nyongo ndio hu...

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA

UGONJWA WA NGIRI AU HERNIA Hernia mara nyingi huwapata wanaume, Wengi waliokumbwa na ugonjwa huu hukosa tiba sahihi na kujikuta wanaangukia kwenye kufanyiwa upasuaji (Operation). Ugonjwa wa ngiri hujitokeza wakati sehemu ya utumbo inapoteleza na kupenya katika kiwambo cha msuli wa utumbo, na kuingia katika kende moja wapo, au sehemu ya juu ya paja. Pia hujitokneza pale kiwambo cha msuli unaotenganisha mapafu na utumbo kinapotoboka na kusababisha majimaji kwenye sehemu ya juu ya utumbo au sehemu ya chini ya mapafu. AINA ZA NGIRI Kutokana na tabia ya ugonjwa wa mshipa wa ngiri kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya mwili, kwahiyo aina ya ngiri/Hernia hutegemea na sehemu ngiri ilipojitokeza: ▪️ Ngiri maji. -Hii ni aina ya ngiri ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama (hydrocele) ▪️Ngiri kavu (Hernia). -Hujulikana pia kama ‘fermoral hernia’ kwa wanawake na huitwa ‘scrotal hernia’ kwa wanaume ▪️ Ngiri ya kwenye kifua - Hujulikana pia kitaalamu kama ‘hiatus hernia’ ▪️ Ngiri ya tumbo -hujulikana p...