Kwa kawaida, mizunguko ya hedhi hukaa kwa siku nne hadi saba. Kwa mfano matatizo ya mzunguko wa hedhi ni Pamoja na mizunguko ambayo hutokea chini ya siku 21 au Zaidi ya siku 35, ukakosa hedhi siku tatu au Zaidi, na mtiririko wa damu ya hedhi ambayo ni nyingi na ya muda mrefu sana au kutokwa na damu ya hedhi nyepesi kuliko kawaida.
Je, Mzunguko Wa Hedhi Wa Kawaida Ukoje?
Wanawake wengi wanapata kipindi cha hedhi ambacho huchukua siku nne hadi saba. Kipindi cha hedhi cha mwanamke kwa kawaida hutokea kila siku 28, lakini mzunguko wa kawaida wa hedhi unaweza kuanzia siku 21 hadi 35.
Mfano wa matatizo ya mzunguko wa hedhi ni kama hii:
- Vipindi vya hedhi ambavyo hutokea chini ya siku 21 au Zaidi ya siku 35
- Kukosa hedhi vipindi vitatu au mfululizo
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi au nyepesi kuliko kawaida
- Kipindi cha hedhi ambacho hukaa kwa muda Zaidi ya siku saba
- Vipindi vya hedhi ambavyo huambatana na maumivu, kichefuchefu au kutapika
- Kutokwa na damu ya hedhi mara mbili kwa mwezi au matone yad amu kujirudia mara kwa mara, au baada ya kukoma hedhi au baada ya tendo la ndoa
Mfano wa mzunguko wa hedhi usio wa kawaida ni Pamoja na:
- Kukosa hedhi kabisa
- Kupata damu ya hedhi na maumivu makali
- Kutokwa na damu ya hedhi kwa muda mrefu
- Kupatwa na damu ya hedhi mfululizo
Je, Nini Visababishi Vyake?
Kuna visababishi vingi vya vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida, kuanzia msongo wa mawazo mpaka magonjwa mengine mbalimbali kama vile:
- Msongo wa mawazo
- Vidonge vya uzazi wa mpango
- Vivimbe kwenye mfuko wa uzazi(fibroid)
- Maambukizi katika via vya uzazi(PID)
- Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
- Mayai kutokupevuka
Visababishi vingine vya mzunguko wa hedhi usio wa kawaida ni Pamoja na
- Saratani ya kizazi au shingo ya kizazi
- Matatizo ya tezi ya thyroid na kupelekea homoni kubadirika
- Madhara yakiambatana na ujauzito au mimba kuharibika au kutunga nje ya kizazi
Je, Hali Ya Kubadirika Kwa Hedhi Hupimwaje?
Kama hali yoyote mzunguko wa hedhi imebadirika, unapaswa kuweka kumbukumbu ujue ni lini kipindi chako cha hedhi kilianza na kuisha, Pamoja na kiwango cha mtiririko na kama unatokwa na damu yenye mabonge. Weka alama ya dalili zozote zingine, kama vile kupata hedhi mara mbili kwa mwezi na hedhi yenye maumivu makali.
Kwahiyo daktari anaweza pia kuagiza upate vipimo hasa vifuatavyo:
- Vipimo vya damu ili kuona upungufu wad amu
- Uchafu unaotoka ukeni ili kuangalia maambukizi
- Kipimo cha ultrasound ili kuona kama kuna vivimbe vya fibroid au kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts)
- Kipimo ili kuona kama kuna tishu zimeota nje ya mfuko wa uzazi
Mpendwa msomaji naomba niishie hapa katika makala hii, na nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATsAP tutakuunganisha na darasa letu uweze kupata masomo kila siku ya afya.
Je, Unahitaji Huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hizi: 0755162724
Dar es salaam-Ilala Boma,
Karibu sana!
Comments